ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 22, 2012

WAKAZI WA MBEYA WAFURIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA SOKOINE STADIUM


Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya.


Mashabiki kibao.

Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond akiwaimbisha mashabiki na wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani Mbeya.

 Shemejiii....Wema Sepetu akiwachetua kidogo wapenzi wa mambo ya filamu.

Msanii wa bongofleva kutoka THT,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.




Wadau wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu.

Watu kibao ndani ya sokoine usiku huu.

Mmoja wa wasanii mahiri wanaotikiza kwenye anga ya muziki wa bongofleva hasa katika miondoko ya R&B,Ben Paul akikamua vilivyo jukwaani huku mashabikiwa wake wakishangilia kwa shangwe. 

Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya  Mh. Dkt. Norman Sigallah akimtaja mshindi wa gari aina ya Vits itolewayo na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemo mojawapo ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,anayeshuhudia ni Meneja masoko wa Push Mobile Rugambo Rodney na kulia ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ,ambapo  katika bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa,aliyeibuka mshindi ni   Eva B Mgovani. 

ni full kujiachi tuu ndani ya uwanja wa sokoine usiku huu.
Pichani kati ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya  Mh. Dkt. Norman Sigallah akiwa katika picha ya pamoja na Meneje vipindi wa Clouds FM,na mdau mwingine.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anaefananishwa na mashabiki wake kama Ray C,aitwaye Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 
Mashabiki wakishangilia vilivyo usiku huu,huku makamuzi ya wasanii yakiendelea jukwaani.
Msanii wa bongofleva anaetikisa kwa nyimbo kadhaa ikiwemo,Mama halima,Aifora na nyinginezo akiwaimbisha mashabiki wake kama waonekanavyo pichani usiku huu.
Mkali mwingine anaekuha juu katika mambo ya kuchana a.k.a kughani Stamina akiamsha kitim kitim kwa wakazi wa mji wa Mbeya usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.