ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 22, 2012

CHEREKO LA 'SEND OFF' YA VERONICA STIMA LAFANA, TABORA

Bibi Harusi mratajiwa Veronica Stima akiwa amesindikiza na kaka yake John Stima kuingia katika ukumbi kwa ajili ya sherehe ya kumuaga (Send Off) iliyofanyika Student Centre, Tabora. Ambapo Harusi yake ni Jumamosi Septemba 22, 2012.

Baba na mama yake mzazi Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza nyimbo ya kikabila la Kifipa.
Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini kwa madaha.
Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake aliomsindikiza katika sherehe yake ya send off iliyofanyika ukumbi wa Student Centre, Tabora.
Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica Stima akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene
Wachanga nao hawakuwa nyuma kuonyesha umoja wao na ule wimbo wao wa kushikana mikono.

Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica Stima wakienda mbele kwa ajili ya utambulisho.
...akilishwa keki na mtarajiwa wake
Bibi harusi mtarajiwa akiaga wazazi wake, kujitayarisha kuungana na mwenzake
...hapa bibi harusi mtarajiwa alikuwa akitoa keki kwa mama mkwe wake mtarajiwa huku kaka yake akiwa amemsindikiza.
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba bibi harusi mtarajiwa akitoa machache.

Mama Catherine Stima ambaye ni mama mazazi wa bibi harusi nae alipata wasaa wa kutoa machache kwa mwanae.

Kaka mkubwa John Stima akiongea machache kabla ya kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Alisema, 'Nawakabidhi dada yangu mpendwa, hana hata doa... nawaombeni msije mkanyanyasa'.
...mara baada ya kuongea machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi.

Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake.

Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyopna mwenyewe.
Picha ya kumbu kumbu kwa wake na watoto wao. Nguzo zote za shughuli hiyo zimedizainiwa na na kushonwa na mwanamitindo Manju Msita

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.