Polisi wakizozana na walinzi wa kikao hicho cha CHADEMA |
Vurugu hiyo iliyotokea majira ya saa 6 :42 za mchana katika ukumbi wa hoteli ya Ladson iliyopo maeneo ya Bwiru Wilayani Ilemela ambapo kundi kubwa la vijana wanaodaiwa ni wafuasi wa chama hicho wakitoka kata ya diwani aliyeenguliwa uanachama Henry Matata walipovamia na kufanya vurugu kubwa na kusababisha hali kuwa mbaya na viongozi hao kuwaita Polisi ambao awali walishauri viongozi hao kuahilisha kikao hicho kutokana na kuwepo ukiukwaji wa amri hiyo ya Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza.
Maafikiano hayakupatikana... |
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilemela (OCD) Debora Magrigimba alipofika eneo la uchaguzi saa 4:00 asubuhi akiwa ameambatana na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa wilaya Magesa hiyo wakiwa na barua ya Mahakama Kuu iliyosainiwa na Jaji Sumar, ya tarehe 14 septemba mwaka 2012 iliyokuwa inaelekeza chama hicho kumshirikisha mwanachama wake huyo kuendelea na harakati zake za kuwania nafasi ya Meya hadi hapo kesi ya msingi itakapomalizika katika Mahakama hiyo.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa wilaya Magesa (aliyenyoosha mkono kulia) licha ya kuwasihi wadau hao wa CHADEMA kufuata amri ya mahakama hakuna aliyetii.... |
Polisi hao walilazimika kuondoka mara baada ya viongozi wa uchaguzi huo kukaidi amri ya mahakama. |
Utata ulizuka pale viongozi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Highness Kiwia na Madiwani waliokuwa waalikwa katika kamati hiyo ya Utendaji ya Wilaya na kushikilia msimamo wa kutoingiza jina la diwani Matata kufanyiwa usaili ili ashiriki kugombea nafasi ya Meya.
Kundi la vijana likitinga lango la kikao cha uchaguzi wa CHADEMA kufanya vurugu. |
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ilemela Yunus Chilongozi amewataka wanachama wa chama hicho kuwa watulivu...
Kijana huyu ametiwa nguvuni kuhusishwa na sakata hilo...
Hali ya usalama iliimarishwa hatimaye wajumbe mmoja baada ya mwingine walitoka ukumbini na kutawanyika. |
Mbunge wa wilaya ya Ilemela jijini Mwanza Highness Kiwia akitoka eneo la uchaguzi huku akipewa ulinzi. |
Mbunge Highness Kiwia akizungumzia sakata hilo mbele ya ofisi za CHADEMA wilaya ya Ilemela ... Sikiliza...
Hivi karibuni madiwani wawili Henry Matata wa kata ya Kitangili na Bw. Adam Chagulani wa kata ya Igoma walitinga mahakamani kupinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama na Kamati kuu ya CHADEMA wakidai kuwa uamuzi wa kuwatimua ulikiuka taratibu za chama hicho na katiba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.