ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2016

CCM KIRUMBA YACHUKUWA HATUA KUKOMESHA MAJI YANAYOHARIBU TASWIRA NJIA ZIINGIAZO UWANJANI HAPO.

Ndugu wadau wa Michezo Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla!
Uongozi wa Uwanja wetu wa CCM kirumba, umeanza kuchukua hatua za kukomesha maji yanayoharibu taswira ya uwanja wetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, zaidi wananchi waliokuwa wakilima katika eneo la Uwanja kwa kuamua kujitolea kuchimba Mkondo wa maji waliouathiri wao kwa shughuri zao za kilimo.
Tumepata ahadi ya Mifuko 10 ya Cement kutoka kwa Wajasiliamali na Mafundi Garage wa eneo la uwanja na jirani, uhitaji ni Mifuko 100 ya Cement, Mawe trip 20, Kokoto trip 3 na Mchanga trip 10, tunaamini kuwa vifaa hivi vikipatikana tutaanza ujenzi haraka wa Mkondo wa Maji ulioathiriwa na Shughuri za Binadamu (Kilimo).
Pamoja na Changamoto nyingi zilizopo, tunaamini kadri siku zinavyosonga tutaendelea kuongeza bidii na maarifa kukabiliana nazo ikiwezekana kuziondoa kabisa au kuzipunguza sana.
Ombi letu kwa wadau wa Soka, tushikirikiane kwa hali na mali kuziondoa changamoto hizo, ili kukifanya kiwanja chetu kuendelea kuwa sehemu muhimu na Salama kwa Michezo.
"Tunaamini katika uwajibikaji na Weredi katika kuwatumikia"
Ndimi Mtumishi wenu:-
S.E.Shija Meneja CCM Kirumba Stadium

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.