ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2016

KIPINDI CHA TAARABU 'SEGA LA LEO' TOKA JEMBE FM CHASABABISHA TABASAMU KWA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU FOREVER ANGEL.

Meneja wa BOA Bank Tawi la Mwanza Bi. Lilian (kulia) akikabidhi mchango wake kwa wadau wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  ili ukabidhiwe kwa kituo cha kulea watoto cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela mkoani Mwanza
 Meneja msaidizi wa Vipindi Jembe Fm Mr. G. Sengo (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mchango wa Kipindi cha KAZI NA NGOMA  kwa mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA' Bi. Fatuma Salum ili ukabidhiwe kwa kituo cha kulea watoto cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela mkoani Mwanza, wa kwanza kushoto ni mweka hazina Nasra Hassan, na kulia ni katibu wa kikundi Ayoub Said.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akikabidhi baadhi ya zawadi za msimu wa sikukuu kwa kituo cha Forever Angel.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimkabidhi unga wa ngano Bw. Hassan ambaye ni Meneja wa kituo cha kulea watoto wadogo cha Forever Angel kilichopo Bwiru wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kama sehemu ya kusherehekea msiku wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya 2017.
'TEAM SEGA' na zawadi zao.
Mwenyekiti wa nidhamu Mustapha Kinkulah Master ambaye pia ni mtangazaji wa Jembe Fm akiongoza shughuli za ukabidhi wa zawadi ambao umefanyika chini ya usaidizi wa wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela, Kampuni ya Startimess, BOA Bank, na wadau wengine wengi walioguswa.
Meneja wa BOA Bank Tawi la Mwanza Bi. Lilian akitoa neno la shukurani jinsi gani alivyoguswa kujitoa kwaajili ya watoto wakituo hicho.
Marafiki wa Jembe Fm wa ndani na nje ya nchi nao hawakubaki nyuma kushiriki nasi kuhakikisha watoto wanaifurahia siku yao.
Keki yakuukaribisha mwaka kituo cha kulea watoto wadogo iliyoandaliwa na TEAM SEGA kwa hisani ya Jembe Fm 93.7
Jiografia ya eneo la tukio.
Kila mdau wa TEAM SEGA alijibidiisha na mtoto wake.
Sasani muda wa kukata keki.
Nilishe nikulishe ya viongozi.
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimlisha keki Meneja wa BOA Bank tawi la Mwanza Bi. Lilian.
Sasa ni zamu yamama mlezi.
Wadau marafiki wa Jembe Fm na TEAM SEGA.
Tamu..........
Mwenyekiti wa Wadau na wanachama wa kipindi cha muziki wa taarab 'Sega la Leo' kutoka Jembe Fm  wanajiita 'TEAM SEGA'  ambaye ni msikilizaji mahiri Bi. Fatuma Salum akimlisha keki Meneja wa kituo cha Forever Angel Mr. Hassan.
Mwenyekiti msaidizi wa TEAM SEGA ambaye ni mtangazaji Johari Ngassa akimlisha keki mmoja wa watoto wa kituo.
Upendo wa dhati 
Sasa ni zamu ya G Sengo.
PAMOJA SANA.
Ni raha tele kituoni hapa kwa siku ya leo.
Mazingira ya ndani kituoni.
MSOSI TIME.






Tunawashukuru wadau wote kwa kutumia muda wenu na nafasi zenu kuhakikisha hili linafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.