Pambano lilianza kwa Nunes kurusha makonde mfululizo kwa Rousey yaliyomwelemea na kuchakazwa ndani ya sekunde 48 tu za pambano hilo na kumfanya mwamuzi, Herb Dean asitishe pambano.
Rousey hakuamini kama angeweza kudundwa katika muda huo mfupi na kuna wakati alitaka kuanguka wakati amesimama kutafakari kilichotokea ndani ya sekunde chache tu.
Hilo linakuwa pigo jingine kubwa katika ungwe ya upambanaji wa bondia huyo ambaye mwaka uliopita alipoteza tena pambano jingine dhidi ya Holly Holm kwa fedheha kubwa.
Swali ambalo watu wengi wanajiuliza sasa ni iwapo Ronda ataendelea tena ngumi ama ataamua kustaafu kabisa.

Referee Herb Dean alijongea na kulisimamisha pambano hata kabla ya pambano kufikisha dakika moja baada ya Ronda kupelekewa makonde ya haja.
Kamwe katika usiku huo Rousey hakumpa kabisa wakati mgumu Nunes ndani ya ulingo zaidi ya kujitahidi kuzuia na kukwepa makonde ya mpinzani wake ambaye hata hivyo ilimchukuwa sekunde 48 tu kudhihirisha ubabe wake.
Rousey akisaidiwa kuondoshwa kwenye ulingo na mama yake, AnnMaria, baada ya kupoteza pambano mapema katika mpambano ulioganyika ijumaa usiku saa za Marekani na alfajiri saa za Afrika Mashariki.
Nunes akisherehekea ushindi na safu yake ya mafunzo na uwezeshaji mara baada ya kutajwa kuwa yu mshindi wa pambano mkanda wa UFC.
Mpiganaji huyo wa ki-Brazil almaarufu 'Simba Jike' alikuwa na ari kubwa na kila dalili ya ushindi maratu sekunde za awali zilipoanza za pambano hilo lililofanyika mjini Las Vegas's stunning T-Mobile Arena.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.