ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 18, 2019

INAOGOFYA - UNYANYASAJI NA VITENDO VYA UKATILI HUANZIA NYUMBANI...!!?



PAMOJA na kuwacha huru watoto wao kujiamulia na kufanya wanavyofanya, ni kwanini wenzetu mataifa ya mbele wameliweza suala la kuwadhibiti watoto wao kimaadili nasi tunaowabana na kuwachunga tukashindwa? 

Kila siku tunasema na kufundisha namna mtoto akipata tatizo shuleni au mtaani mahala sahihi pa kukimbilia ni kwa wazazi, walezi au kwa waalimu lakini tunasahau kumwelekeza mtoto huyo huyo, wapi pa kukimbilia pale anapopata tatizo linalichangiwa na wazazi, walezi au familia.

Jeh wazazi wanapata changamoto gani katika kutoa elimu kwa watoto wetu?

Kwa kuliona hilo Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ya Tanzania na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa UnfPA pamoja na UN WOMEN wameandaa semina ya siku tatu kwa walimu wa shule za sekondari na msingi wilayani Sengerema kuwafundisha mbinu na namna ya kuwasaidia watoto wanaokabiliana na changamoto za vitendo vya ukatili kutoa elimu ya Afya kujitambua kwa jinsi na jinsia kwa wanafunzi wa darasa la 2 hadi wanafunzi wa sekondari kidato cha 4.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.