ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 16, 2019

MTOTO AMCHOMA KISU NA KUMUUA MTOTO MWENZAKE KISA DENI LA SHILINGI MIA MBILI



Kutoka eneo la vilima vya mtaa wa Mkudi, Ghana kata ya Nyamanoro B jijini Mwanza mwanafunzi wa darasa la 6 Shule ya msingi Ghana aliyetambulika kwa jina la Saleh Bundala ameuawa kwa kuchomwa shingoni na kitu chenye ncha kali na kijana mwenzake (jina limehifadhiwa) katika ugomvi wa kudai shilingi za kitanzania mia mbili (200/=) 

Kwa mujibu wa vijana waliokuwa karibu na tukio lililotokea juzi Jumapili ya tarehe 14 mwezi April 2019 majira ya saa 9 alasili, wanasema kuwa marehemu alikuwa amesimama pembeni akiwatizama vijana wenzake waliokuwa wakicheza kamari na mshitakiwa alisikika akilalamika kuwadai wenzake shilingi 200/= aliodai wamemdhulumu.

Akiwa na hasira mtuhumiwa alianza kumpiga 'makwenzi' bila sababu mtoto mdogo ambaye alikuwa amesimama pembezoni akishangaa mchezo  huo ndipo marehemu Salehe akauliza kwanini unampiga mdogo wangu? Mvutano ukatokea penye kuamua, kijana mtuhumiwa akamshindilia Salehe Bundala kitu chenye ncha kali shingoni damu zikaanza kutiririka kwa wingi ......hali iliyo sababisha kifo. 

Siku hiyo hiyo ya tukio (juzi Jumapili) mara baada ya kutokea mkasa huo wa kusikitisha na kuogofya KAZI NA NGOMA ya Jembe Fm ilidhuru eneo husika kuzungumza na mashuhuda pamoja na baba mzazi wa marehemu kujua Kisa na Mkasa.......

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.