ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 19, 2019

ZANTEL YAPATA VYETI VYA KIMATAIFA VYA ISO VYA MAZINGIRA, AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI


Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imepata vyeti 2 vya ubora wa kimataifa (ISO), kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa katika  kutekeleza kwa ufasaha kuendesha biashara zake kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira  (ISO 14001:25),na cheti kipya cha utekelezaji wa  mifumo ya Afya na Usalama mahali pa kazi (ISO 45001:2018).

Mafanikio haya ni mwendelezo, mwaka jana mwishoni baada ya kufanyiwa ukaguzi ilipata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kukidhi vigezo vya utekelezaji mifumo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwa ufasaha (OHSA 18001:2007).

Kutokana na ukaguzi huo, ilibainika inatekeleza vizuri mifumo ya Afya na Usalama, wakaguzi walipendekeza ZANTEL ibadilike kutoka cheti cha zamani cha OHSA 18001:2007 na kupatiwa cheti kipya cha ISO ambacho kimeanza kutolewa kwa makampuni yanayokidhi vigezo mwaka jana.

Akiongelea mafanikio haya ya kampuni kupata vyeti vya kimataifa vya ISO,Mkuu wa kitengo cha Teknolojia  Mawasiliano wa Zantel,John Sicilima alisema “Tunayo furaha kukidhi viwango vya ukaguzi na kupewa vyeti vya ubora vya kimataifa.Hatua hii inadhihirisha umakini wetu tunavyozingatia suala la afya na Usalama kuanzia kwa wafanya kazi ,wadau mbalimbali tunaoshirikiana nao  na  katika mazingira tunayofanyia shughuli zetu,kama malengo yetu tuliojiwekea mojawapo ni kuendesha shughuli zetu tukiwajibika kulinda usalama wa jamii katika maeneo tunayofanyia biashara sambamba na kuongeza hadhi ya kampuni yetu”.

Alisema baada ya kupata vyeti vya kimataifa vya ISO, Zantel itahakikisha inafanikisha dhamira yake katika maeneo ya afya na tahadhari katika usalama, athari za mazingira, Kutekeleza kanuni za usalama kwa vitendo, mifumo ya uharibifu wa mazingira wa sauti na kuhakikisha tahadhari zaidi na athari zinadhibitiwa ipasavyo.

“Utekelezaji wa maelekezo yanayoendana na vyeti hivi yatawezesha taswira ya Zantel kuwa nzuri zaidi, kuongeza uhusiano mzuri na jamii na kupanua wigo wa masoko ya biashara zetu na wadau wengine,” aliongeza Sicilima.

Cheti cha kimataifa cha ubora cha ISO 45001 taasisi yenye kuwa nacho, inapaswa kuwa inatekeleza mifumo ya Afya na Usalama kwa ufasaha, lengo kuu likiwa ni kulinda Afya na usalama kwa wafanyakazi na watu wengine.

Utoaji wa cheti kipya cha ISO 45001, umeanza mwezi Machi mwaka 2018, kuhakikisha kanuni za Afya na Usalama zinapewa kipaumbele duniani kote. Taasisi ya Kimataifa ya Kusimamia Ubora (ISO) imelenga kuhakikisha matukio ya ajali na magonjwa yatokanayo na shughuli za kazi yanapungua sambamba na kuwezesha umri wa kuishi kuogezeka.

Kutokana na kuanza kutolewa kwa cheti cha ubora cha kimataifa cha ISO 45001, taasisi ambazo zilikuwa katika mfumo wa cheti cha zamani cha ISO ikiwa ni pamoja na cheti cha OHSAS 18001 yanapaswa kubadilika na kupata cheti kipya kabla ya kufikia mwezi Machi mwaka 2021.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.