Picha ya moja ya hukumu zilizosomwa mwaka 2010 ikimuonyesha aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza Bihondo (kushoto) na watuhumiwa wengine (waliofunika nyuso). |
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imewaachia huru watuhumiwa wanne akiwemo aliyekuwa meya wa jiji la mwanza LEONARD BIHONDO waliokuwa wakikabiliwa kesi ya mauaji ya aliyekuwa katibu wa CCM kata ya isamilo marehemu BAHATI STEPHANO aliyeuawa kikatili mei 14 mwaka 2010 kwa kuchomwa kisu katika ziwa lake la kushoto akiwa ofisini kwake katika eneo la Nera jijini Mwanza.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011 Jaji mfawidhi wa mahakamu kuu kanda ya Mwanza AISHIEL SUMARI amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri umeshindwa kuwatia hatiani washitakiwa wote wanne na hivyo kuwaachia huru.
Jaji SUMARI amesema kuwa maelezo ya shahidi namba 16 na 18 ambao walikuwa askari polisi waliokabidhiana mtuhumiwa namba moja ulikuwa na mkanganyiko kutokana na hatua ya Jamhuri kushindwa kumpeleka mahakamani aliyekuwa mkuu wa polisi wilaya ya Nyamagana THADEO MALINGUMU ambaye angeweza kuondoa mkanganyiko huo kuhusu mtu aliyechukuliwa na Polisi na mtuhumiwa aliyetolewa ziwani.
Amesema kuwa ushahidi uliotolewa na Jamhuri ni utambuzi wa mahakamani na siyo wa eneo la tukio ambapo mahakama haiwezi kumtia hatiani mshitakiwa huyo wa kwanza ambaye awali alipatikana na kesi ya kujibu.
Kuhusu washitakiwa wengine BALTAZAR SHUSHI, ABDUL AUSI pamoja na mshitakiwa wa nne aliyekuwa meya wa jiji la mwanza LEONARD BIHONDO ambao waliunganishwa kwenye kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011 baada ya kutajwa na mshitakiwa wa kwanza jaji SUMARI amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri umeshindwa kuwatia hatiani.
Jaji SUMARI ametolea mfano hatua ya jamhuri kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyothibitisha kuwepo kwa mawasiliano ya simu baina ya mshitakiwa wa kwanza JUMANNE OSCAR na mshitakiwa wanne LEONARD BIHONDO.
Kutokana hali hiyo,Jaji Sumari amesema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri kuwa haukuwatia hatiani na hivyo kuwaachia huru washitakiwa wote wanne na kutoa fursa kwa upande wa jamhuri kukata rufaa ikiwa haujaridhika na uamuzi huo wa mahakama.
Bahati Stephano aliyekuwa katibu wa CCM kata ya isamilo aliuwawa kikatili mei 14 mwaka 2010 kwa kuchomwa kisu katika ziwa lake la kushoto akiwa ofisini kwake katika eneo la nera jijini mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.