ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 8, 2011

KAMA SERIKALI YENYEWE HAIZITHAMINI MAKTABA ZAKE WANANCHI WATAJENGA VIPI TABIA YA KUJISOMEA?

Kuna kale kamsemo ambako kiukweli sikaendi lakini ntafanyaje 'ishakuwa' Kanasemaaaa: 'UKITAKA KUMFICHA MWAFRIKA WEKA UJUMBE KWENYE KITABU' Uskute kamsemo haka virusi vyake vimeenea hadi ngazi za juu za wasemaji wa taifa hili (viongozi tulio wachagua na walio teuliwa).Jengo la maktaba kuu Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Mazingira ya maktaba kuu ya Wilaya ya Kwimba iliyoko mkoani Mwanza ni picha mbaya hasa kwa sekta ya elimu ya Taifa hili, inatia aibu sana hasa ukizingatia kuwa hii ni sehemu ya kujisomea kwa wilaya hii mama ambayo imekuwepo tangu miaka ya 60 ikikuza kata zake kimaendeleo na hatimaye kata hizo kugeuzwa kuwa wilaya.

Katika maktaba hii vitabu ni vichache visivyojitosheleza iwe katika nyanja za elimu au mambo mbalimbali yanayoihusu nchi yetu Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla hata vitabu vilivyopo kuhusu elimu ni vya kale mitaala ya zamani (visivyotumika).

Mtangazaji wa Star Tv, Rogers William na kitabu cha Nyerere.

Pamoja na kasoro zote kiukweli maktaba hii ina vitabu fulani vya historia la taifa letu vyenye mafunzo thabiti, adimu sehemu nyingine kuvipata, vitabu hivi vingejumuishwa na vingine vinavyotoka miaka ya sasa mbona elimu ingesonga.

Eti haya ndiyo magazeti latesti!!

Siku natembelea maktaba hii ilikuwa ni tarehe 1june 2011 na Gazeti 'latest' linalosomwa maktabani hapo ni la tarehe 4may 2011.

Bango la sheria za maktaba.

Hili ndilo dirisha.

Jengo limechakaa na kuwa makazi ya popo na njiwa wasio na makazi, jengo halina ulinzi kiasi kwamba kuna kipindi uvamizi ulitokea ambapo wezi hao waling'oa nondo mbili za dirisha hili kisha wakapenya kuiba vitendea kazi muhimu ikiwa ni pamoja na vitabu.

Dirisha la maktaba wilaya ya Kwimba kwa nje.

Kwa ndani.

Viti vya kukaa wasomaji jamani ni aibu tupu! Viongozi na watendaji hakuna anayethubutu kufika hapa kusoma vitabu japo hupita maeneo haya na kuona sura ya maktaba ilivyo hoi’ kwani hutumia eneo hili kama njia ima kuelekea maofisini mwao au kuelekea uwanjani kwa shughuli za makusanyiko.

Maji yanasiku nyingiiiiii...Nalo Sinki la kukoshea mikono limegeuka kuwa chombo cha kuhifadhia kadi za wanachama wa maktaba.

Mkutubi

Kwa mujibu wa maelezo ya mkutubi wa maktaba: wanafunzi wa secondary pekee ndiyo huwa wanafika kujisomea huku wakikumbana na changamoto ya kukosa vitabu kwa baadhi ya masomo, ni nadra kwa wilaya nzima kufikia wastani wa wanafunzi 30 kwa siku wanahudhuria maktaba hii!

BIG UP's KWA
Christopher Kangoye - Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.
Shahbani Mtarambe - Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Kwimba.
Bila kusahau Wizara ya elimu.

@g.sengo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.