ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 11, 2011

MWANAHARAKATI, MPIGANIA UHURU WA AFRIKA YA KUSINI MAMA ALBERTINA SISULU AZIKWA LEO.

Sala ya maziko ya mama Albertina Sisulu, mfuasi mashuhuri wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, imehudhuriwa na watu wengi Soweto pamoja na watu mashuhuri wa nchi hiyo na nje akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Zuma alitaka Bibi Sisulu apewe mazishi ya kitaifa ambapo majenerali walibeba jeneza la mama Sisulu katika ibada hiyo iliyofanywa kwenye uwanja mkubwa wa michezo wa Soweto, ambako Rais Jacob Zuma aliongoza maombolezi.

Alisema: "Enzi imemalizika, na taifa limeondokewa; lakini tuna fahari kwamba tukimjua Mama Albertina Sisulu.


Baadhi ya wakazi wa soweto waliohudhuria mazishi ya mpigania uhuru Albetina Sisulu yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto leo (picha na Freddy Maro)

Tunamzika shujaa na mama wa taifa. ambaye alikuwa jabari na imara katika kupambana na ukandamizi wa ubaguzi wa rangi, huku akiwa na huruma kwa maskini na wanyonge.

Hapo awali, Nelson Mandela alisema Bibi Albertina Sisulu alikuwa mmoja kati ya wazalendo wakubwa wa Afrika Kusini. Bwana Mandela alikuwa mpambe kwenye harusi ya Bi Albertina na hayati Walter Sisulu - ambaye alimshawishi Mandela ajiunge na chama cha ANC..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.