::BAJETI::
Serikali imepandisha bei katika vinywaji baridi, bia, sigara, mvinyo, vinywaji vikali, tumbaku, faini kwa makosa ya usalama barabarani (notification).
Serikali itasamehe VAT kwenye vipuri vya zana za kilimo; chakula cha kuku; nyuzi zinazotumika kutengeneza nyavu za kuvulia samaki; kwenye vipuri vya mashine za kunyunyiza na kutifua udongo na mashine za kupanda nafaka.
Waziri wa Fedha na Bajeti 2011/12.
Mkulo amesema inapendekezwa kufanyiwa marekebisho ya kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya kuendeshea mitambo kutoka Sh 80 hadi Sh 40 kwa lita, ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa nchini:- Bidhaa hizo ni vinywaji baridi kutoka Sh 63 kwa lita hadi Sh 69 kwa lita; bia inayotengenezwa na nafaka ya nchini na ambayo haijaoteshwa, kutoka Sh 226 kwa lita hadi Sh 249 kwa lita.
Bia nyingine zote, kutoka Sh 382 kwa lita hadi Sh 420 kwa lita; mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka Sh 1,223 kwa lita hadi Sh 1,345 kwa lita.
Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, utatozwa Sh 420 kwa lita; vinywaji vikali kutoka Sh 1,812 kwa lita hadi Sh 1,993 kwa lita.
Kurekebisha viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye sigara ambavyo ni sigara zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka Sh 6,209 hadi Sh 6,830 kwa sigara 1,000.
Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75 kutoka Sh 14,649 hadi Sh 16,114; sigara nyingine zenye sifa tofauti na hizo za awali kutoka Sh 26,604 hadi Sh 29,264 kwa sigara 1,000.
Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara kutoka Sh 13,436 hadi Sh 14,780 kwa kilo na ushuru wa siga unabaki asilimia 30. Kwa mujibu wa Mkulo, hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh milioni 99,521.5.
Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye mnagari ya mizigo yenye uwezo zaidi ya tani 20; kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya 25 kwenye mabasi yanayoingizwa kwa ajili ya mradi wa mabasi ya Jiji la Dar es Salaam, na kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye pikipiki maalumu za kubeba wagonjwa.
Hatua hizo za kodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa kuanzia Julai mosi, isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo. jumla ya Sh bilioni 13,525.9 zinahitajika kutumika katika kipindi hicho cha mwaka 2011/12
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.