NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando jijini Mwanza imepokea vifaa tiba vya upasuaji wa ugonjwa wa fistula ya uzazi kutoka shirika la Americares, vyenye thamani ya shilingi milioni 234.2 vitakavyosaidia utoaji huduma ya matibabu ya ugonjwa huo. Akizungumza Juni 01, 2023 kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema vitasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa akina mama wanaougua fistula ya uzazi na hivyo kuzuia vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.