WAKAZI
wa Mtaa wa Kagomu na maeneo ya Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana wamemtaka
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomon Kibamba kuacha kutengeneza migogoro ya
ardhi katika maeneo yao na badala yake apeleke watalaam wake kupima maeneo yao
kama alivyoagizwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivi
karibuni alipokuwa katika ziara yake ya kikazi.
Hayo
yalijitokeza jana wakati wa mkutano wa hadhara wa Diwani wa Kata ya Mahina,
James Bwire (CCM) ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza uliofanyika katika mtaa wa
Kagomu wakimuomba Meya huyo afatilie agizo la Waziri William Lukuvi alilolitoa
wakati alipofanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo kutokana na muda
aliotoa wa upimaji shirikishi kuwa mdogo ili hali bado wataalamu awajafika
kuwapimia.
Martine
Magoma akihoji wakati wa maswali kwa Diwani Bwire alisema kwamba muda
uliotolewa na Waziri Lukuvi wa Jiji kupima maeneo ya wananchi ni mdogo ambapo
mwisho ni Juni 6 mwaka huu lakini hadi sasa wataalamu wa Idara ya Mipango Miji
kitengo cha upimaji hawajawahi kuonekana na wananchi hawajui nini kinaendelea
na wananchi wako tayari kulipia gharama za Sh 150,000/- za upimaji shirikishi.
Akijibu
maswali ya wananchi Meya Bwire alisema kwamba atalifikisha kwa Mkurugenzi ili
wataalam wafike kuja kuwapimia na kinachotakiwa ni kujiandaa kulipia gharama
hizo kwa kuwasiliana na wenyeviti wa mitaa yenu na Mtendaji wa Kata na hili
litasaidia kuanza utaratibu wa kumilikishwa maeneo ya makazi yenu kama
alivyoagiza Waziri Lukuvi.
Meya
akihutubia wananchi wa mtaa huo alikataa la Mwenyekiti wa mtaa wa Igelegele,
Dancan Nyamgoncho (CHADEMA) kwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata
(WDC) na maswali yake anatakiwa kuuliza huko na kumtaka akaye chini awachie
wengine, akieleza kusikitishwa kwake na
Mkurugenzi wake wa Jiji kutaka kutengeneza mgogoro wa ardhi hilo akitumia
mwenyekiti mmoja (hakumtaja) kudai eneo langu ninalojenga Hospitali kuwa ni
mali ya wananchi.
“Kuna mambo yanaendelea pale Jiji ambayo
baadhi ya wataalam na watumishi wamekuwa na tabia ya kutafuna fedha za
Halmashauri ikiwemo kufanya mambo ya hovyo, sasa tangu nimechaguliwa kuwa Meya
nilikaa na Madiwani wenzangu na kukubaliana kukataa Jiji letu kuwa shamba la
bibi kwa kuchotwa fedha za walipa kodi kutumika kinyume cha utaratibu kamwe
hili sitokubaliana nalo,”alisema.
Bwire
alieleza kuwa nachojua Mkurugenzi ni Mtendaji siyo mwanasiasa hivyo ache
kutuingilia wanasiasa na kutufatafata kwa kutaka kutuchonganisha na kuturetea
migogoro ya ardhi badala yake afanye kazi ya kupima maeneo yetu kama
alivyoagizwa na Waziri na kama anahitaji eneo langu basi anilipe fidia na
kulichukua awape watu anaowahitaji lakini siyo kuanza kutengeneza visa baada ya
kumkatalia ulaji kule Jiji.
Naye
Mwalimu Steven Machunda akijitokeza katika mkutano huo na kueleza kuwa eneo
analojenga Meya Hospitali ni eneo lake halali kwa kuwa baba yake mzazi na yeye
waliamua kumuuzia mwaka 2009 ili kupata fedha wakati anashinda kwenda Chuo cha
Ualimu Mrutunguru kutokana na kukosa fedha mwanzoni ndipo familia ikamua
kumuuzia kihalali na kumukabidhi nyaraka zote.
Machunda
alisema kwamba hata baada ya kumaliza Chuo na kupata ajira amekuwa akipata msaada kutoka Meya kama mtu
ambaye alimpatia mwanga hivyo kama kuna mtu anadai eneo hilo ni lake ajitokeze
hapa ili ni muone na kumuhoji hali iliyoibua shangwe kwa wananchi na kumuonya
mkurugenzi huyo kuacha kumchonganisha na kiongozi huyo mpenda maendeleo na
badala yake atafute njia nyingine ya kumchafua.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.