WANACHAMA
na mashabiki wa timu ya Yanga Africans Jijini Mwanza wameandaa sherehe na chakula
cha usiku baina yao, wachezaji na viongozi wa juu wa Klabu hiyo watakaoambatana
na timu eneo la Villa Park Resort baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi kuu ya
Vodacom (VPL) utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Akizungumza na GSENGO BLOG Mjini Mwanza, msemaji wa tawi la Mwanza lililopo mtaa wa Rufiji, Sele Yanga maarufu kama 'Lialia' alisema kwamba uamuzi huo umefikiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa ushirikiano na umoja uliowezesha kutwa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo.
Akizungumza na GSENGO BLOG Mjini Mwanza, msemaji wa tawi la Mwanza lililopo mtaa wa Rufiji, Sele Yanga maarufu kama 'Lialia' alisema kwamba uamuzi huo umefikiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa ushirikiano na umoja uliowezesha kutwa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo.
Sele
alisema kwamba baada ya sherehe hiyo siku ya Jumapili wachezaji, benchi la
ufundi na viongozi walioambatana na timu jijini Mwanza watashiriki katika
uzinduzi wa matawi mawili ya Mwanza mjini na Mecco majanini lililopo Nyakato
ikiwa ni sehemu ya pili ya mashabiki kupiga picha na wachezaji wa timu na
viongozi sanjari na kuongeza hamasa na kuwaaga kabla ya kurejea jijini Dar es
salaam.
“Tunataraji
kuwa na mapokezi makubwa pale uwanja wa ndege wa Mwanza siku timu itakapowasili
kuja kucheza na timu ya Mbao FC ya Jijini Mwanza katika mechi ya mwisho ya
kufunga msimu wa Ligi kuu ya VPL 2016/2017 ambayo Yanga Africans inatwa taji la
Uchampioni kwa mara ya tatu mfululizo, rai yangu kwa wanachama na mashabiki
wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba,”alisema.
Naye
Meneja wa Burudani wa Villa Park Resort, Ramadhan Maganga alikiri kuwa na program ya kuandaa chakula cha usiku (Dinner) kwa
viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga
Africans ambapo kwa wanachama na mashabiki watakaotaka kujumuika kwa chakula na
wachezaji na viongozi watachangia gharama kidogo.
Maganga
alisema kutakuwa na eneo maalum limeandaliwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa
mashabiki na wanachama ya kupiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi ambapo
mlangoni wataingia kwa kuchangia Sh 3,000/- na kutakuwa na burudani ya muziki
kutoka katika bendi ya Villa Park ya Super Kamanyola .
Meneja huyo
alisema kwamba tayari wameisha toa taarifa kwa barua kwa viongozi wa Klabu hiyo
Makao Makuu na kupewa rukusa hiyo ambapo watashirikiana na viongozi na wanachama
wakiwemo baadhi ya mashabiki kuanda shughuli hiyo na kutoa wito kwa mashabiki
kuzikiliza utaratibu kupitia vituo mbalimbali vya redio na magazeti kujua nini
watafanya kabla ya kujumuika na wachezaji na viongozi katika sherehe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.