aibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi
Maryam Juma Abdullah (aliyesimama) akiwakaribisha ugeni kutoka Benki ya
Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB).
Mjumbe
wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo
(aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
Mkuu
wa Msafara wa TADB, Bibi Rehema Twalib (katikati) ambaye pia ni Mjumbe
wa Bodi wa Benki hiyo akihimiza jambo wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni
Mjumbe wa TADB, Bw. Hussein Mbululo na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili
Bibi Maryam Juma Abdullah (kulia).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (aliyesimama)
akieleza dhima ya Benki ya Kilimo katika kusaidia juhudi za Serikali
katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini Tanzania.
Mkurugenzi
wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kushoto)
akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati
walipotembelea viongozi na wajumbe wa Bodi ya TADB
walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Mipango wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar,
Sera na Utafiti, Bw. Sheha Idrissa Hamdan (aliyesimama kushoto)
akizungumza wakati Ugeni wa Benki ya Kilimo
ulipotembelea wizarani hapo.
Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Na Mwandishi wetu,
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imeanza kuchangamkia fursa za
uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo visiwani Zanzibar kwa kuanza
mchakato wa kutoa mikopo kwa wakulima
na wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha katika uchakataji wa mazao
ya kilimo visiwani humo.
Akizungumza
wakati wa walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi,
visiwani humo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis
Assenga alisema kuwa TADB ikiwa chombo
cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika
kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri
zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya
kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya
asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
“Uanzishwaji
wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija
kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya
dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba
nafuu
ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.
Bw.
Assenga amesema Zanzibar ina utajiri mkubwa kwenye uzalishaji wa viungo
‘spices’ ambayo ni mojawapo wa minyororo ya thamani ya mwanzo
inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani
mazao mbalimbali na Benki ya Kilimo.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na
Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah ameishukuru Benki hiyo kwa
kuiangalia Zanzibar kuwa sehemu ya kimkakati na
kutaka kuanza mikopo visiwani humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.