ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2017

POLISI YA AFRIKA KUSINI YAANZISHA UCHUNGUZI WA VISA VYA MAUAJI YA WANAWAKE.

Polisi nchini Afrika Kusini imeanzisha uchunguzi kuhusiana na kile kinachoonekana kama mlolongo wa mauaji ya wanawake kwenye mtaa wa Soweto mjini Johannesburg.

Uchunguzi huo wa polisi ya Afrika Kusini umeanza baada ya kuripotiwa visa kadhaa vya mauaji dhidi ya wanawake. Polisi wa mji wa Guateng wanafanya uchunguzi baada ya miili ya wanawake wanne kupatikana mwishoni mwa wiki katika eneo eneo hilo, jambo ambalo limezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia hususan wanawake.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, tayari miili mitatu ya wahanga wa mauaji hayo imeshatambuliwa.
Bongeka Phungula na Popi Qwabe walitoweka siku ya Ijumaa na inaripotiwa kuwa pia walikuwa wamebakwa.
Kikosi cha polisi cha kupambana na uhalifu nchini Afrika Kusini
Mwili wa Lerato Moloi ulipatikana eneo la Naledi huko Soweto, huku mwili wa nne ukipatikana eneo la kutupa takataka. Raia wengi waliohojiwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini wameonesha wasiwasi mkubwa wa mauaji hayo ambayo inaonekana kuwa, wahanga hao wamekuwa wakibakwa kabla ya kuuawa.
 
Radio za Afrika Kusini zimepokea simu nyingi kutoka kwa raia wa nchi hiyo wanaoitaka serikali kuchukua hatua za haraka za  kupambana na uhalifu na kufanya jitihada za kuwalinda wanawake na watoto wa nchi hiyo.
Wanawake waliouawa hadi sasa wana umri usiozidi miaka 30. Hayo yanajiri katika hali ambayo, wanaume 11 jana walifikishwa mahakamani mjini Johannesburg wakihusishwa na mkasa wa utekaji nyara na mwanamke mmoja mjamzito aliyebakwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.