ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 18, 2017

JAMBAZI SUGU LANASWA MKOANI NJOMBE.

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia mtu mmoja anaefahamika kwa jina la Balton Mangula anaetuhumiwa kwa matukio mbalimbali yakiwemo ya mauaji na uporaji kwa kutumia silaha.

Mtuhumiwa Balton Mwenye umri wa miaka thelethini na saba ambae ni mkazi wa kijiji cha ilongelo ambae amekamatwa kijijini huko kwa tuhuma za matukio mbali mbali ambapo baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi cha makambako ambapo baada ya kukamatwa alikiri kuwa anamiliki silaha mbili pamoja na risasi ambavyo ni kinyume na sheria.

Aidha akibainisha majina ya silaha zilizokamatwa kamanda wa polisi mkoa wa njjombe Podensiana Protas amesema silaha hizo ni pamoja na Uzgun Namba 3052 ikiwa na Magazine yake wakati silaha ya pili ni Chinese PISTO yenye namba AC0963 ikiwa na magazine yake.

Kamanda protasi ameendelea kuvieleza vyombo vya habari kuwa baada ya mtuhumiwa kueleza ukweli aliweza kueleza mahali alipozificha silaha hizo ambazo zilikuwa zimefichwa katika kijiji cha kitandililo kwenye korongo lililoko mlima fiho ambapo ndipo alipozificha silaha hizo.

Hata hivyo kamanda wa polisi ameeleza kuwa mtuhumiwa Balton Mangula amekuwa akitafutwa tangu mwaka 2015 kuhusiana na matukio mbalimbali aliyokuwa ameyafanya yakiwemo ya unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na mauaji huku akibainisha baaadhi ya maeneo ambayo mtuhumiwa amefanya matukio hayo huku akiongeza kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapo kamilika.

Wito umetolewa kwa jamii kuhusu kutoa taarifa pindi wanapo baini mienendo mibaya ya watu wanaoishi nao katika maeneo yao ili kunusuru mali na maisha yao dhidi ya majambambazi hao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.