PRESS RELEASE
MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO
Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara
amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa
Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara
hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe
yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia
amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na
ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi(Mapambo)
yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na
Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na
hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi
hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.