ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 18, 2013

AKUMAKI WAOMBA UFADHILI KUNUSURU MAZINGIRA YA MJI WA PANGANI

Hii ni sehemu moja wapo ya ufukwe wa bahari katika eneo la wilaya ya Pangani mjini katika eneo la makutano ya mto Pangani na bahari ya Hindi.
Hali ya ufukwe ni mbaya sana na hatarishi kwa maisha ya wakazi wa mji wa Pangani.

Ufukwe huo unaathirika na mmomonyoko wa udongo kwa fukwe hiyo ya bahari, uharibifu wa mazingira na kuanguka kwa miti aina ya Mivinjea na Mikoche katika sehemu hiyo.
Uharibifu mwingine unasababishwa na kuzagaa taka ngumu zikiwemo chupa za plastiki, mifuko ya nailoni na taka nyingine zinazotupwa na wapitanjia wakiwemo wasafiri watumiao usafiri wa majini pamoja na wakazi wa mji wa Pangani ambao hutupa taka hizo baharini nazo mwisho wa siku zikizagaa ufukweni.
Wana AKUMAKI pamoja na wataalamu  wa Halmashauri ya mji wa Pangani wakiwa katika ukaguzi wenye madhumuni ya kufanya jitihada za kunusuru hali hiyo ya uharibifu wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya mji wa Pangani.
AKUMAKI wanawaarifu wadau wengine kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha juu ya suala zima la kuhifadhi mazingira na usafishaji wa fukwe zetu zote hapa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na upandaji miti ya asili yenye kuhifadhi mazingira yakiwemo majani aina ya Mla kasa.
Hali ya mazingira inatatanisha, mti mmoja baada ya mwingine unapuputika kuukaribisha ukame nayo bahari kukosa ulinzi.
Kwa kukosa miti ardhi inatafunwa (inamomonyoka) na kupoteza rutuba yake.

Wana AKUMAKI wana karibisha makampuni mbalimbali yenye malengo ya kurejesha faida kwa jamii katika kufadhiliwa miti nao wakiwatayari  kufanya zoezi hilo kwa kujitolea. 

Ufukwe ni  moja ya vivutio kwa wageni kama inavyoonekana katika picha, watalii wakiwa baharini katika mji wa Pangani eneo la ufukwe wa Funguo (PAndedeco) wakifurahia maadhari.

Je wewe wafurahia wageni kama hawa wakute sehemu zetu adimu zikiwa duni. 
Mazingira na yatunzwe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.