Na Mwandishi Wetu.Morogoro
NAIBU waziri wa habari utamaduni na Michezo Amos Makalla ameikabidhi timu ya taifa ya pool table bendera ya taifa kwaajili ya kwenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya afrika mashariki nchini Malawi,ambapo aliwataka kwenda kuitangaza nchi kwa mema.
Makala alikabidhi bendera hiyo jana mjini Morogoro na kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa raia wema ili wengine waweze kuiga kutoka kwao sambamba na kuonyesha umoja na ushirikiano.
Alisema Serikali imeanza kuutambua mchezo huo na kuupa ushirikiano hivyo kuipongeza kampuni ya TBL kupitia bia yake ya safari lager ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa mchezo huo.
“ Hongereni TBL kwa kazi nzuri mnayoifanya huu mchezo ulikuwa haufahamiki kabisa na sasa unajulikana na kupendwa ni kazi kubwa ambayo mmeifanya inayostahili kuigwa na makampuni mengine” Alisema Naibu Waziri huyo.
Naye Mwalimu anaeinoa timu hiyo alisema anaishukuru timu hiyo kwa kuwa imekuwa ikionesha nidhamu ya hali ya juu tangu wakiwa kambini, nakwamba timu imejiandaa vya kutosha na wanauhakika wakurudi na ushindi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa pool table Tanzania (TAPA) Fredy Mushi aliiomba serikali iuangalie mchezo huo badala ya kungalia michezo mingine, nakwamba kufanya hivyo kutawawezesha wachezaji kuwa na ari ya kufanya vyema zaidi wakati wamashindano kama haya.
Aidha wachezaji wanaokwenda kushiriki michuano hiyo nchini Malawi ni , Kampten watimu hiyo Vernace Charles, Omary Akida, Festo yohana, Mohamed Idd, Mercxedek Amedius,Godfrey Swai, Abdala Husein, na Patrick Mnyanguzi.
Mashindano hayo ambayo yanataji kuanza kutimua vumbi Oktoba 23 hadi 26 yanatarajia kushirikisha nchi 14 kutoka afrika ambazo ni Kenya , Tanzania,Afrika ya Kusini,Zambia, Lesotho,Kongo, Swazland, Ghana,,Nigeria, Misri, Morocco, Namibia, Msumbiji, na Mwenyeji Malawi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.