ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 16, 2013

BONANZA LA MICHEZO KWA WATUMISHI ILEMELA

BONANZA LA MICHEZO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA LAFANA      
Bonanza la michezo lililojumiuisha zaidi ya  watumishi 200 wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutoka Idara zote kuanzia ngazi ya Shule, Kata na Makao Makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela lilifanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 12.10.2013 katika viwanja vya michezo vya shule ya Sekondari Buswelu na kufunguliwa rasmi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mh. Henry Matata. Bonanza hili lilijumuisha michezo ya mpira wa Miguu (Football) wanaume, mpira wa Pete (Netball) wanawake, mpira wa wavu (Volleyball) kwa wanaume na wanawake na Riadha kwa wanaume na wanawake.

Akisoma risala fupi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Afisa Utamaduni wa Manispaa, Bi. Rosemary Makenke alielezea lengo hasa la Bonanza hili ikiwa ni:
·         Watumishi kujumuika pamoja na kufahamiana.
·         Watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali ya Soka, Netball, Volleyball na Riadha ili kujenga afya za miili yao.
·         Kusheherekea kwa njia ya michezo kutimia kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela tarehe 01.10.2012.
·         Kupata nafasi ya kuchagua wachezaji watakaounda timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inayotarajiwa kwenda kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA katika Manispaa ya Dodoma kuanzia tarehe 21.10.2013.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, Mstahiki Meya alisisitiza yafuatayo:
·         Watumishi wote kuanzia wakuu wa Idara na wale wanaowaongoza washiriki katika michezo kwani ni sehemu kubwa ya kufahamiana ambayo huja kuleta ufanisi katika kazi kwani  michezo hutumika kama sehemu ya kupunguza migogoro katika jamii.
·         Atashauriana na Mkurugenzi kutenga bajeti ya kutosha ya michezo ili kuweza kukidhi mahitaji muhimu yanayoitajika kama vile vifaa vya michezo (mipira, jezi na viatu), huduma ya kwanza, maji ya kunywa n.k.

Katika bonanza hili ambalo lilionekana kuwa na upinzani mkubwa na ilidhihirshwa pale timu zilizocheza mchezo wa fainali soka kufikia hatua ya penati, timu shiriki ziliundwa kama ifuatavyo:
1.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
2.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
3.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
4.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.

Matokeo ya michezo ilikuwa kama ifuatavyo:
MPIRA WA MIGUU (FOOTBALL)
1.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
2.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
3.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
4.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.

MPIRA WA PETE (NETBALL)
1.      Kata ya Pasiansi na Ilemela
2.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
3.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.
4.      Kata ya Bugogwa na Sangabuye.

MPIRA WA WAVU (VOLLEYBALL) – WANAUME.
1.       Kata ya Bugogwa na Sangabuye.
2.      Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
3.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa
4.      Kata ya Pasiansi na Ilemela

MPIRA WA WAVU (VOLLEYBALL) – WANAWAKE.
1.       Kata ya Kirumba, Nyamanoro na Kitangiri
2.      Kata ya Nyakato, Buswelu na Makao Makuu ya Manispaa.


RIADHA:
WANAUME ROUND 1: MITA 100
1.       Samson Msodoki
2.       Mahamba Sebastian
3.       Msema Ernest
WANAWAKE ROUND 1: 100
1.       Frola Masatu
2.       Devotha Bukulu
3.       Kissa Mwakibinga
WANAUME MITA 800 WANAUME

  1. Yusuph Mboje
  2. Joshua Nassari
  3. Antidius Selestin

WANAUME ROUND 2: MITA 100
1.       Albert Mongela
2.       Nyawabu Maganga
3.       Said Wawa
WANAWAKE ROUND 2: 100
1.       Edith Shekifu
2.       Felista Kilasa
3.       Veronika Tesha



MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA                                                                                         


Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mh. Henry Matata akihututubia wanamichezo mbele ya waandishi wa habari kutoka TBC, CHANNEL 10, STAR TV, BARMEDAS TV, RFA, CLOUDS FM,METRO FM na AFYA RADIO.
Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Ndg. Kizito Bahati akifafanua mbele ya waandishi wa habari malengo ya uanzishwaji wa Bonanza la michezo katika Manispaa ya Ilemela.
Sehemu ya umati wa watumishi wanamichezo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi waBonanza la Wafanyakazi.
Refarii wa mechi ya ufunguzi Siraji Tuwa  akihesabu hatua za miguu 12 kwa ajili ya penati ya ufunguzi iliyopigwa na mgeni rasmi huku golikipa  Gido Buretta  akijitayarisha kudaka.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya, Mh. Henry Matata akisalimia na Wilbard kutoka timu ya Makuu Makuu wakati wa mechi ya ufunguzi rasmi wa Bonanza la Wafanyakazi. 
Baadhi ya wachezaji kutoka Makao Makuu wakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni  Hamis, David, Hashimu, Mutani na Goodluck, 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Alhaj Zuberi Mbyana akiwa na Shilinde wakiteta jambo wakati wakiangalia mechi ya mshindi wa  3
Baadhi ya picha za timu shiriki katika Bonanza la Michezo la Manispaa ya Ilemela.                                                                                                                                                                                                                                                                               

Imetolewa na:
Kizito I. Bahati

Afisa Michezo - Manispaa ya Ilemela.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.