ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 20, 2010

KUHUSU MAUAJI KAMANDA SIRO ANASEMA......

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SIMON SIRO Akisema:-
“Jana jioni majira ya saa 10 pale uwanja wa ndege wa Mwanza tuliweza kumkamata mh. Leonard Bandiho Bihondo ambaye ni mstahiki meya wa jiji la mwanza ana umri wa miaka 64 kwa tuhuma hii ya mauaji ya Bi Bahati Stephano aliyekuwa katibu wa ccm isamilo jijini Mwanza, hii imekuja mara baada ya kufanya mahojiano na watuhumiwa wote watatu ambao tayari tumekwisha wakamata, wote wamekuwa wakimtaja kwamba ndiye anaye husika katika tukio hili. Kwahiyo mahojiano yanafanyika ili tuweze kujua ukweli wa tuhuma hizi na kama tutathibitisha bila mashaka kwamba anahusika na mauaji haya either kwa kula njama au kwa njia nyingine basi tutampeleka mahakamani na sheria kuchukua mkondo wake. Lakini niombe kwamba bado tunahitaji taarifa nyingine nyingi maana tunajua suala la kesi ya mauaji ni kubwa na linahitaji ushahidi ulio mkamilifu toka pande zote mbili kwa lengo la kuhakikisha kwamba hatutomwonea mtu yeyote ili kulinda haki ya kila mtu na kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliyeko juu ya sheria.”
****Tukio la mauaji ya Bahati lilizua mjadala mkubwa huku mauaji hayo yakihusishwa na masuala ya kisiasa.

Inadaiwa kuwa hivi sasa makundi yanayohasimiana ndani ya CCM yanachuana kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Waliokwisha kukamatwa ni pamoja na Jumanne Oscar (30) ambaye anatuhumiwa kumchoma Bahati kwa kisu sehemu za tumboni na kwenye titi na kusababisha kifo chake. Oscar alikamatwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa kabla ya kukamatwa kwa Bihondo jana, ni Baltazar Shushi ambaye mwaka 2009 aligombea uenyekiti wa mtaa wa Isamilo Kaskazini B kwa tiketi ya CCM na kubwagwa na mgombea wa Chadema.

Kada mwingine aliyekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ni pamoja na Abdul Ausi aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Isamilo kabla ya uchaguzi wa 2007.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.