Mhifadhi mkuu wa hamba la miti la Sao Hill Lucas Sabida akiongea na waandishi wa habari juu ya utalii huo mpya wa mchezo wa mbio za magari katika msitu wa shamba hilo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wakala wa huduma za misitu Tanzania
(TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill mkoani Iringa wameanzisha utalii wa
michezo ya magari katika shamba hill kwa lengo la kuunga mkono juhudi za
kutangaza utalii wa ndani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alivyofanya kwenye filamu ya Royal Tour.
Akizungumza wakati wa kutangaza kwa
mashindano ya magari katika shamba la miti la Sao Hill, Mhifadhi mkuu wa shamba
hilo Lucas Sabida alisema kuwa wamejipanga kuanzisha utalii katika shamba hilo
ambao utaongeza kipato kwa wananchi na shamba hilo.
Sabida amesema kuwa kwa sasa
wameanzisha utalii wa mchezo wa magari ambao unatarajiwa kufanyika tarehe
11/09/2022 katika shamba la miti la Sao Hill na wananchi wote wanakaribishwa
kwenda kutazama mchezo huo.
Alisema kuwa wao kama Shamba mbali na
kujihusisha na shughuli za mazao ya isitu lakini pia wanafanya shughuli za
utalii wa michezo ambapo kwa mara ya kwanza wameanza na utalii wa Mbio za
Magari ambayo yatafanyika September 11 Mwaka huu.
"Leo tumekutana kwa lengo la
kujiridhisha na kuangalia maandalizi hatua ambayo tumefikia hadi sasa sanjari
na kukagua njia zote ambazo zitatumika kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu ni
zoezi ambalo halijawahi kufanyika katika historia ya shamba letu hivyo ni kitu
kipya." Amesema Sabida
Sabida alisema kuwa katika Shamba
hilo kuna barabara ambazo wamekuwa wakidhihifadhi ambazo zinaurefu wa
kilometer 1500 hivyo ni fursa ya kipekee ya kutumiwa kwa utalii wa michezo
ambayo ni mchezo mpya
kwa upande wake Mwenyekiti wa
Mbio za Magari kwa Mkoa wa Iringa Amjad Khan amesema kuwa Sao hill na wao
kwa pamoja wameshirikiana kuandaa Mashindano hayo madogo ya magari ambayo
huitwa sprint kwa ajili ya kujifunza kuhusu Shamba hilo
" Hadi sasa tumejipanga vizuri
na maandalizi yamefikia asilimia 99 kwa sababu tulijipanga vizuri ili
kuhakikisha Mashindano hayo yanafanikiwa kwa sababu tulianza kujiandaa
mwezi mmoja na nusu kabla ya siku hii ambayo tunazungumza na waandishi
ikiwa kila kitu kimekamilika." Amesema Khan
Amesema kuwa Mashindano hayo ni fursa
nzuri kwao ya kushirikiana na Serikali kuweza kutangaza msitu huo ili watu
waweze kuelewa zaidi pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kutangaza
masuala ya utili ikiwa utalii wa michezo.
"Malengo ya Mashindano hayo ya
magari ni kutangaza msitu wa sao hill hivyo Iringa motorsports Club
tumepata fursa hii hivyo .. Sisi kama club tumefurahi sana... Kwa bahati ambayo
tunaipata na tumeipokea kwa mikono miwili na tunajisikia furaha
sana." Amesema Khan
Naye Mchezeshaji wa mchezo huo
wa magari John Makeo alisema asilimia kubwa wamepata ushirikiano mkubwa
kutoka kwa shamba kwakuwa ni mara ya kwanza kushiriki michezo huo katika Shamba
hilo.
"Watu wengi wa Mafinga walikuwa
wanakuja Iringa kwa ajili ya kuangalia Mashindano hayo lakini September
11 yatafanyika katika Msitu wa shamba la Sao hill ambapo wataweza kujionea
fursa zilizopo na kuzitangaza ikiwemo utalii wa nyuki pamoja na gundi zipo
katika msitu hii" Amesema Makeo
Hata hivyo katika Mashindano hayo
jumla ya madereva zaidi ya 20 wanatarajiwa kushiriki katika mchezo huo
ambapo hadi sasa wanajumla ya washiri 14 ambao wamekubali kushiri kwenye mchezo
huo watazungumza mizunguko minne ambayo Sawa na kilometer 6.
Sabida amesema kuwa SAO HILL MISITU AUTO CROSS ni zao jipya la Utalii ndani ya Shamba la Miti SaoHill Mafinga TFS wanasema utalii wa aina hii ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya Shamba la Miti SaoHill
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.