ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 8, 2022

VIDEO TFS WAJA NA MASHINDANO YA MAGARI

 Wa kwanza kwenye video ni Mhifadhi mkuu wa shamba la miti la Sao Hill Mufindi Lucas Sabida anayefuata ni mwenyekiti wa Rally Iringa anaitwa Amjad khan



Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill mkoani Iringa wameanzisha utalii wa michezo ya magari katika shamba hill kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kutangaza utalii wa ndani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyofanya kwenye filamu ya Royal Tour.

Akizungumza wakati wa kutangaza kwa mashindano ya magari katika shamba la miti la Sao Hill, Mhifadhi mkuu wa shamba hilo Lucas Sabida alisema kuwa wamejipanga kuanzisha utalii katika shamba hilo ambao utaongeza kipato kwa wananchi na shamba hilo.

Sabida amesema kuwa kwa sasa wameanzisha utalii wa mchezo wa magari ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 11/09/2022 katika shamba la miti la Sao Hill na wananchi wote wanakaribishwa kwenda kutazama mchezo huo.

Alimesema kuwa lengo kubwa ni kuanzisha mashindano makubwa ya mbio za magari Africa kwa kuwa wanabarabara ambazo zinahimili hilo na zina urefu wa kilomete 15000


Sabida amesema kuwa SAO HILL MISITU AUTO CROSS  ni zao jipya la Utalii ndani ya Shamba la Miti SaoHill Mafinga   TFS wanasema utalii wa aina hii ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya Shamba la Miti SaoHill

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.