ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 8, 2022

MALKIA ELIZABETH ALAZWA KWA MATIBABU.

 


Kasri la Buckingham nchini Uingereza limetangaza kuwa kiongozi mkuu wa kimila wa nchi hiyo, Malkia Elizabeth yupo chini ya uangalizi maalumu wa matibabu kwenye kasri la Balmoral nje ya jiji la London kutokana na maradhi ambayo hayakuwekwa wazi.


Taarifa hiyo iliyotolewa leo Septemba 8, imesema madaktari wa Malkia wamependekeza abaki chini ya uangalizi wa matibabu.


“Malkia anaendelea vizuri na yuko Balmoral kwa matibabu na mapumziko," imesema sehemu ya taarifa hiyo.


Hali hiyo imemtokea malkia huyo mwenye umri wa miaka 96 ikiwa ni siku chache tangu akutane na Waziri Mkuu anayeondoka madarakani Boris Johnson kabla ya kumteua waziri mkuu mpya, Liz Truss.


Pia, kutokana na mwenendo wa afya yake malkia Elizabeth alilazamika kuahirisha kikao chake na Baraza la Mawaziri kilichotakiwa kifanyike siku ya jana, Septemba 7, 2022 baada ya kushauriwa na madaktari wake kupumzika.


Nchi hiyo inaongozwa kwa mfumo wa serikali ya kifalme huku makao makuu yake yakiwa kwenye kasri kuu la Buckingham lililopo kwenye jiji la London, hata hivyo kasri lingine ambalo malkia amepelekwa kupumzika lipo Balmoral eneo la Aberdeenshire huko Scotland.   


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.