NA ALBERT G. SENGO
MWANZA. Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi Mhe. Angeline Mabula amesema mpaka sasa jumla ya watu 2,700 kati ya 3500 tayari wameshapata viwanja vyao, huku baadhi yao wakiwa na hati walizopata papo hapo na wengine wakisubiri kukamilisha malipo ili wapewe hati zao. Ndani ya viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza watumishi wa vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya Ardhi wilaya ya Ilemela wameweka kambi hapa kutoa huduma zote katika eneo moja. HUDUMA ZINAZOTOLEWA 1. Kwa uuzaji wa viwanja vilivyotangazwa, mnunuzi atakwenda kwenye ramani na kuchagua kiwanja, atapewa bei kupitia mtandao, atalipa na kupewa hati ya kumiliki papo hapo. 2. Kwa wanaotaka kulipa kodi ya ardhi hakuna riba kwa msamaha wa Rais Samia. 3. Huduma zote zinazotolewa na ofisi ya ardhi zinapatikana hapa kwani hii ni One Stop Centre.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.