ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 5, 2022

TBS YAWANOA MAAFISA BIASHARA NA AFYA PWANI

 Na Victor Masangu,Pwani 

Serikali mkoani Pwani imewataka watumishi wa halmashauri hususan maafisa afya na biashara kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika kudhibiti ubora wa bidhaa zinazozalishwa ziwe na viwango vinavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Zuwena Jiri wakati kufungua mafunzo ya siku moja kwa watendaji wa halmashauri tisa za Mkoa wa Pwani juu ya kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa majukumu ya ushirikiano wa na Shirika la viwango wa Tanzania (TBS)

Katibu huyo aliongeza kuwa watumishi hao wanapaswa kuyatumia vema mafunzo hayo waliyoyapata katika kuwahudumia wananchi wote ambao wapo katika halmashauri zao na kwamba katika suala zima la kuhakiki ubora wa bidhaa.

"Azma ya serikali ni kwa ajili ya kushughulikia mambo mbali mbali ya udhibiti wa bidhaa ambazo zinazalishwa ikiwemo bidhaa vipodozi pamoja na chakula pamoja na biashara kuwa na viwango vya hali ya juu,"alisema Katibu huyo.

Pia maafisa wa afya pamoja na maafisa biashara inatakiwa wawe na sifa na kuzingatia maadili na miongozi yote katika kukabiliana na udhibiti wa bidhaa mbali mbali hivyo serikali itaendelea kushirikiana na Tbs ili kutoa elimu zaidi kwa watumishi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Dkt. Ngenya Yusuph amebainisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa  watumishi ili waweze kupata fursa ya kuwahudumia wananchi katika suala la udhibiti ubora wa bidhaa.


Aidha alifafanua mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo zaidi watumishi wa halmashauri hizo za Mkoa wa Pwani katika suala zima la kueaelimisha wananchi wa ngazi za chini kuhusiana na udhibiti wa ubora wa bidhaa zao.

"Leo tupo hapa Wilayani Kibaha na sisi Kama tbs kwa kushirikiana na serikali tumeona Kuna umuhimu mkubwa wa kuwakutanisha maafisa wa  afya na biashara katika kuwapatia elimu juu ya udhibiti ubora wa bidhaa katika vipodozi na masuala ya chakula,"alisema Mkurugenzi huyo.


Nao baadhi wa washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wamedai yataweza kuwaongezea ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao.



Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamewashirikisha maafisa biashara na maafisa afya kutoka halmashauri zote Tisa za Mkoa wa Pwani yameandaliwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.