ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 5, 2022

RUTO ASHINDA KESI YA UCHAGUZI, NDIYE RAIS ANAYESUBIRI KUAPISHWA.

Philomena Mwilu (kushoto) na Martha Koome wakati wa moja ya mikutano ya kusikilizwa kwa kesi ya urais.

 Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo Martha Koome hatimaye ametangaza kuafiki uamuzi wa ushindi wa Rais Mteule William Ruto, kwenye kesi iliyowasilishwa na muungano wa Azimio la Umoja. 

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, Koome alisema kwamba makamishna wanne waliojitenga na kutangazwa kwa matokeo ya mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hawakuwa na ushahidi kwamba uchaguzi wa Agosti 9 ulitiwa doa. 

Vile vile Jaji Mkuu alidokeza kuwa ushahidi wa John Githingo haukuafikia viwango vinavyotakikana. 

Wakati huo huo mgombea urais wa Azimio Raila Odinga ameposti picha akifuatilia mwenendo wa kesi hiyo ya uchaguzi kwa njia ya television.

 

Raila alikuwa amesema kuahirishwa kwa chaguzi hizo ulikuwa ni njama ya mahasimu wake kwa ushirikiano na mwenyekiti, kusababisha watu wasijitokeze kumpigia kura katika maeneo hayo ambayo ni ngome yake.

Tayari shamrashamra zimeanza kulipuka, huku baadhi ya television zikionesha matukio mbalimbali toka viunga tofauti tofauti kwa wananchi wa taifa hilo wakishangilia ushindi wa bwana Ruto.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.