ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 7, 2022

"NITASTAAFU LAKINI KIONGOZI WANGU NI BABA" RAIS UHURU ASEMA.

 


Rais Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kumkabidhi naibu wake William Ruto mamlaka baada yake kuibuka mshindi wa uchaguzi wa urais. 

 Akiongea katika kikao na wabunge wa muungano wa Azimio katika mkahawa wa Maasai Lodge, Uhuru amesema ni wajibu wake kikatiba kufanya hivyo. 

Katika kile huenda kikazua hisia mseto, Rais alisema atafanya hivyo lakini kiongozi wake atasalia kuwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa Azimio. "… nitapeana mamlaka nikiwa natabasamu kwa sababu ni wajibu wangu kikatiba kufanya hivyo, lakini mimi kiongozi wangu ni Baba Raila Odinga," Uhuru amesema. 

 Rais amewakosoa Wakenya kwa kumchagua Ruto akisema wamekataa nafasi ya kuleta umoja nchini. "Mmekataa nafasi ya kuleta umoja humu nchini. 

Si Raila mmenyima nafasi," alisema Rais wakati wa kikao hicho Amewataka viongozi wa Azimio la Umoja kusalia ngangari huku akiwashtumu wale ambao wanaungana na Kenya Kwanza. "Jameni msiwekwe mfuko," alisema akiashiria viongozi ambao wameamua kufanya kazi na muungano wa Ruto. 

Rais alikuwa akiunga mkono Raila kuwa rais wa tano wa kitaifa baada yake kukosana na naibu wake. Wakati wa kikao hicho, alipigia debe Kalonzo Musyoka kuwa Spika wa Seneti akisema wakifaulu kufanya hivyo watakuwa na nafasi ya kuendeleza ajenda za Azimio. 

Sasa Kalonzo watamenyana na aliyekuwa gavana wa Kilifi Amason Kingi ambaye anaungwa mkono na Kenya Kwanza. Katika bunge, Kenneth Marende naye amependekezwa na Azimio huku Kenya Kwanza nao wakiunga mkono Seneta Moses Wetangula. 

Ruto aliibuka mshindi wa uchaguzi wa urais baada ya kujizolea kura 7.1M dhidi ya Raila aliyepata 6.9M.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.