ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 1, 2018

MASWALI MA 5 YA WASHIRIKI MISS LAKE ZONE 2018 KWA JESHI LA POLISI MWANZAGSENGOtV Washiriki wa Shindano la kumsaka Miss Lake Zone 2018 hii leo wameketi meza moja na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi jijini Mwanza wakiuliza na kujibiwa maswali mbalimbali yaliyokuwa yamejikita katika nyanja tofauti tofauti za rika na staha mbalimbali. Pengine wengi twaweza kuwa na maswali:- JEH kitu gani cha msingi walichofuata kwenye ofisi hizo nyeti za Serikali? GsengoTv imekusogezea maswali ya udadisi na yenye tija kwa jamii yaliyoulizwa na warembo hao.
1. Kuhusu bodaboda na kamatakamata ya kutovaa kofia ngumu.
2. Waoto watukutu wanapokamatwa kwa makosa na kuwekwa sero moja na wakubwa
3. Taratibu za mwendo kasi wa uendeshaji na tochi za barabarani.
4. Kesi za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwanini mara nyingi zinaangukia pua.
5. Kesi za uhujumu uchumi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Mkadam Khamis Mkadam ndiye mwenyeji wa wanyange hao na hapa anasimama kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.


Ni mwendo wa kusababisha tabasamu pichani mchango wa Miss lake Zone 2018 kwa Kituo cha watoto wadogo waishio mazingira magumu cha FKT jijini Ilemela Mwanza.
Kuzungumza nao na hata kujua changamoto zao FKT.
Picha ya washiriki Miss lake Zone 2018 pamoja na Kitengo cha Usalama Barabarani na Makosa ya Jinai Polisi Mwanza.
Picha ya pamoja hapa ni walimu na wasimamizi itifaki Miss lake Zone 2018 na Kitengo cha Usalama Barabarani na Makosa ya Jinai Polisi Mwanza.
Utalii Mwanza unaanzia hapa 'SANGARA MTEMA MAJI'
Utalii na mazingira.
Katikati ya jiji la Mwanza.

Watalii nao wamo....Tukutane Jumamosi hii ya tarehe 4 Sept 2018 Rock City Mall Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.