ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 2, 2018

VIDEO:- WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA WAAPISHWA AUGUST 02/2018.GSENGOtV
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya wanne baada ya kuteuliwa Rais Dk. John Magufuli hivi karibuni.

Mongella amewaapisha wakuu hao wa wilaya leo mapema katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa, ambapo waliokula kiapo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Severin Mathias, Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana Dk. Philis Nyimbi, Mkuu wa Wilaya Magu Philemon Sengati na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Kanali Lucas Magembe.

Pia Mongella aliwaomba wakuu hao wa Wilaya kuwa waadilifu katika kazi waliyopata sambamba na  kuongoza wananchi vyema ikiwemo kutatua kero zao bila woga.

"Kupata cheo cha kuwa Mkuu wa Wilaya siyo lazima uwe msomi sana bali ni utendaji kazi wako mpaka Rais akuone wewe amekuamini ndio mana hamjatuma vyeti kwa ajili ya kuomba cheo hichosambamba na uwezo wa Mungu," amesema.


Aidha Mongella amewataka wakuu hao wapya kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kuinua uchumi wa mkoa ambayo inashika nafasi ya tano kati ya majiji sita nchini.Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Philis Micheck Nyimbi akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati Lugumiza akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Lucas Magembe akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hohn Mongella ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mathias Latika akila kiapo cha utumishi tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya yake.
Kiapo kwa pamoja.
Kiapo kwa wakuu wa wilaya za Ukerewe, Magu, Nyamagana na Ilemela mkoa wa Mwanza.
Mbela wanasa matukio taswira ya zoezi la kula Kiapo kwa wakuu wa wilaya za Ukerewe, Magu, Nyamagana na Ilemela mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiendesha utaratibu katika kusanyiko la kuwaapisha wakuu wa wilaya za Nyamagana, Ukerewe, Ilemela na Magu shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi yake.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Tesha alipata fursa ya kuaga na kutoa shukurani kwa viongozi na wadau wenzake aliofanya nao kazi.
Shukuran......
Viongozi.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, mama Khadija Nyimbo akitoa neno mara baada ya kustaafu.
Kutoka kushoto ni wakuu wa wilaya za Ukerewe, Nyamagana Magu, na Ilemela.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Philis Micheck Nyimbi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mathias Latika.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati Lugumiza.
Mhe. Mongella.
Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.
Familia nazo zimehusika kwa ukaribu tukioni.
Mhe. Mongella akichapa neno.
Wasimamizi wa shughuli za ulinzi na usalama.
Kusanyiko la uapisho.
Wazee wa Siasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.