Baada ya hali kiuchumi kuwa ngumu ndani Yanga, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, ametangaza kuomba wanachama mashabiki wa timu hiyo kuichangia fedha.
Kaaya ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ambaye alijiuzulu kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya kiafya, amewaomba wanayanga wajitoe ili kuisaidia timu wakati huu wa mpito.
Kaimu huyo amesema kinachofanyika hivi sasa ni kuandaa namba maalum ambazo wanayanga wataweza kuzitumia kwa ajili ya kuichangia fedha ili kuikwamua klabu hiyo na hali ngumu inayopitia kwa sasa.
Yanga imeamua kufikia maamuzi hayo ili kuweza kupata fedha walau za kuweza kujikimu wakati timu ikiwa kambini kwa ajili ya msimu ujao na mashindano mengine ikiwemo ya kimataifa.
Wakati uongozi ukitangaza kuandaa namba hizo za kuchagia, kikosi cha timu hiyi sasa kipo katika maandalizi ya msimu mpya na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa siku za usoni jijini Dar es Salaam.
CHANZO AZAM TV
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.