Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisomamaelezo ya mmoja ya mtuhumiwa aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituocha Polisi Bunda wakati wa ziara ya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wamashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu waWilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi waandamizi wa kamati yaUlinzi na Usalama wilayani Bunda.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mara, Mrakibu Mwandamizi ,Jeremiah Shila akitoamaelezo ya mwenendo wa mashtaka ya watuhumiwa walioko katika Kituo cha PolisiBunda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi HamadMasauni(wapili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili(watatu kulia),wakati wa ziara ya naibu waziri kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka yamahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatukushoto), akifuatilia wakati mpelelezi akifunua jalada la mmoja wa mahabusualiyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi Bunda wakati wa ziaraya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katikavituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili nawengine ni viongozi waandamizi wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayaniBunda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Serikali Kujenga Nyumba 400 za Askari Polisi Na Mwandishi WetuSerikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zaaskari polisi kote nchini, ikiwa ni kukabiliana na changamoto ya makaazi ya askarina uchakavu wa vituo vya polisi ili kuwawezesha askari hao kutekeleza majukumuyao kwa ufanisi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MhandisiHamad Masauni alipotembelea kijiji cha Makongoro wilaya ya Bunda mkoaniMara kuona changamoto wanazokutana nazo askari polisi katika kutekelezamajukumu yao ya ulinzi na usalama.
Alisema wizara iko katika mpango maalumu wa kuboresha makazi ya askari polisinchini huku akitoa wito na nafasi kwa wadau wa maendeleo pia kujitokeza nakuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli kuboresha makazi ya askaripolisi “Katika kukabiliana na changamoto ya askari nchi nzima tayari tushaanza kujengamakazi ya askari wetu tukianza na nyumba za polisi Kusini Pemba na tutaendeleana ujenzi huo wa nyumba 400 katika mikoa mingine nchini na kutokana na haliniliyoiona hapa Bunda basi tutatoa kipaumbele hapa”Alisema Naibu Waziri Masauni Akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika ujenzi wamakazi ya askari polisi wilayani humo huku Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mussa Masilu akiongeza kuwa nyumba hizo ni chakavu na zinashusha hadhi ya Askari Polisi.
Hadi sasa serikali imeshaanza taratibu za awali ikiwemo tathmini ya ujenzi wanyumba hizo mia nne za askari polisi nchini ambapo mikoa mbalimbali itanufaikana ujenzi huo utakaotekelezwa kwa awamu tofauti ukienda sambamba na ujenzina ukarabati wa vituo vya polisi. ……………………………......................MWISHO………………………………………..
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.