Mwakilishi wa Mandawa AMCOS kutoka Wilaya ya Ruangwa, Selemani Mwigambe, akiwasilisha hoja wakati wa kikao cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na wawakilishi wa vikundi vidogo vya ubanguaji wa korosho kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi. Kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kilikuwa na lengo la kutambua changamoto za vikundi hivyo ili kuviwezesha kushiriki zoezi la kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
Baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya wabanguaji wadogo wa korosho kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakifuatilia kwa makini maelekezo ya serikali yaliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda(hayupo pichani) kwenye kikao chake na wawakilishi hao leo mjini Mtwara.
GSENGOtV
Waziri Kakunda Atoa Maagizo Mazito MtwaraWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda ameziagiza taasisimbalimbali za serikali zihakikishe zinashirikiana kwa pamoja ili kutimiza azma yaserikali kuona wabanguaji wadogowadogo wa korosho wanashiriki kwenye zoezi lakubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
Kwenye kikao chake na wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya kubangua koroshokutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, Waziri Kakunda amewaagiza Makatibu Wakuu wawizara yake na ile ya Kilimo kwa kushirikiana na Makatibu Tawala wa mikoa hiyomiwili, wanahakikisha wabanguaji wadogo wanapewa ushirikiano kwa kupatiwakorosho za kubangua kutoka kwenye maeneo yao.
Kuhakikisha ubora wa korosho itakayobanguliwa na vikundi vya wabanguaji wadogoinakidhi viwango vya soko, mheshimiwa Kakunda amelitaka Shirika la Mendeleo yaViwanda Vidogo (SIDO) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele kwa pamoja wafanyeziara za kutembelea vikundi hivyo ili kujua changamoto zinazowakabili. “Jipangenikuwatembelea kwenye maeneo yao mjiridhishe na kuona teknolojia wanazotumiamuwasaidie inapobidi ili ubora wa korosho itakayobanguliwa ulindwe na uwe mzuri”amesisitiza Waziri Kakunda.
Waziri Kakunda pia ameitaka SIDO ihakikishe inavisaidia vikundi hivyo vya ubanguajimikopo ya mashine itakapothibitika kikundi kina uwezo kufanya kazi lakini hakinavitendea kazi.Kuhusu kilio cha wakulima kudhulimiwa korosho wakati wa kupima, Waziri Kakundaameagiza Wakala wa Vipimo (WMA) ianze mara moja zoezi la kuhakiki mizanizinazotumiwa kwenye maeneo ya kukusanya na kupima korosho.
Waziri Kakundaamesema, “Wakala wa vipimo nchini watembelee maeneo yote yanayofanyaukusanyaji na upimaji wa korosho kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwaniwajiridhishe kama vipimo vinavyotumika vinakidhi matakwa ya kisheria”.
Aidha amewataka Makatibu Tawala wa mikoa wahakikishe wanasimamia utekelezajiwa Sheria ya Ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999 ambayo inazitaka serikali za mitaangazi ya halmashauri kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kila kijiji.
Sheriahizo mbili zimetenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kijamii, kidini nakiuchumi. Utekelezaji wa sheria hizo utawanufaisha wabanguaji wadogo kwa kutengamaeneo watakayo kuwa wanafanya kazi zao bila bughudha.
Kwa upande wao wabanguaji wadogo wamepongeza hatua iliyochokuliwa na serikaliya kununua na kuhakikisha korosho zote zinabanguliwa nchini. “Uamuzi wakushirikisha wabanguaji wadogo ni jambo la kupongezwa sana, hakika Rais Magufuli nikiongozi wa wanyonge” amesema Bi. Daria Erasto, Mtendaji Mkuu wa Umoja waWabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.