ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 10, 2018

10 WAFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA + MGONGO KWA MAFANIKIO BUGANDO


GSENGOtV
Wagonjwa 10 wenye tatizo katika ubongo na mishipa ya fahamu na mgongo wamefanyiwa upasuaji na kukamilika salama katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza.

Upasuaji huo unafanywa na daktari bingwa wa mifupa kutoka Marekani kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati upasuaji huo ukiendelea hospitalini hapo, Daktari bingwa wa upasuaji Isidory Ngayomela, amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto za upasuaji.
Ameongeza kuwa mpaka hapo walipofika wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa watu 10 wale waliopata ajali na kuumia kichwani pamoja na mgongo kupinda kutokana na uzee.
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji kutoka Saint Francis Hospital and Medical Centre ya Hartford nchini Marekani, Dr. Christopher Comey (kulia katika picha juu akiwa na mwanahabari Albert G. Sengo wa Jembe Fm Mwanza) amesema tangu awasili Bugando ikiwa ni wiki moja sasa, wameshafanya upasuaji kwa wagonjwa 10 zikiwemo oparesheni mbili za ubongo.
"Mara kwa mara nimekuwa nakuja nchini Tanzania, kwaajili ya kutoa huduma ya kujitolea lakini safari hii nimeamua kutoa na mafunzo kupitia ujuzi niliona kwa madaktari wa hapa ili huduma ziendelee na hata kama sipo watu wasiendelee kutaabika"
Comey amewasifia madaktari wa Bugando akisema "Pamoja na changamoto ya uhaba wa vifaa na miundombinu mingine nafurahi kuona  madaktari wa Bugando wakichapa kazi kwa bidii maarifa na weredi wa hali ya juu huku wakizingatia kile ninachowafundisha" 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.