ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 2, 2014

DJ STEVE JUNIOR KUTOKA KENYA ATINGA TZ KUKISANUKISHA KESHO IJUMAA VILLA PARK JIJINI MWANZA

Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior akitizama maadhari ya jiji la Mwanza baada ya kuwasili leo mchana kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza.
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior (katikati) akifanya mahojiano na G. Sengo (kushoto) katika hoteli ya JB Belmonte baada ya kuwasili leo mchana kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. Kulia ni Meneja wa Dj Huyo.
WAFANYABIASHARA wanao miliki vituo vya radio, television pamoja na kumbi za burudani nchini wameaswa kuwekeza katika muziki wa reggae kwa kuanzisha vituo maalum vya kupiga muziki huo na kumbi maalum za muziki huo kwani ni sekta ambayo ni fursa iliyo wazi kwa kuwa soko lake lipo si kwa vijana tu bali hata kwa watu wazima.

Hayo yamesemwa na Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior ambaye yuko jijini Mwanza katika ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa barani Afrika akitoa burudani ya muziki huo na kuutambulisha uzuri wake kwa jamii kizazi na kizazi ambapo kesho (Ijumaa) kwa mara ya kwanza atakutana na mashabiki wake pale Villa Park kwenye Tamasha lake linalojulikana kama REGGAE BRING BACK LOVE.

Dj Steve Junior anasema kuwa ni kwa takribani miaka kumi sasa amewekeza katika muziki huo akiburudisha na kuufanya muziki huo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yake, familia na jamii yake. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA MAHOJIANO.

Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior (katikati), Kutoka Clouds Fm G. Sengo (kushoto) katika hoteli ya JB Belmonte baada ya kumaliza mahojiano leo mchana ikiwa ni matayarisho kwaajili ya Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. Kulia ni Meneja wa Dj Huyo.
Dj Maarufu wa muziki wa Reggae kutoka nchini Kenya Dj Steve Junior amefurahia sana mapokezi aliyoyapata toka kwa watanzania wakarimu.
Ni wakati wa ku-Enjoy mazingira safi na tulivu ya jiji la Mwanza yanayo nakshiwa na muonekano wa ziwa Victoria. 
100 usikose Tamasha la REGGAE BRING BACK LOVE litakalo fanyika kesho Ijumaa (3/oct/2014) Villa Park Mwanza. 
Swimming pool iliyo juu ya ghorofa...
With FrendZ...!!
Mpango mzima wa Ijumaa hii tarehe 3/oct/2014

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.