ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 15, 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima. 
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto).
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. a
Pichani meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Pichani meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.