ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 16, 2016

WAZIRI KITWANGA AWAPIGA STOP MAAFISA ARDHI KUVAMIA NA KUPIMA MAENEO YA WANANCHI WILAYANI MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi(CCM), akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Usagara kusikiliza kero na changamoto zilizopo pamoja na kutoa ufafanuzi wa matatizo yao.
Na PETER FABIAN, MISUNGWI.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwnga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi amewapiga stop Maafisa Ardhi kwenda kwenye Vitongoji, Vijiji na Kata kuvamia na kupima maeneo bila kuwashirikisha viongozi na wamiliki wa maeneo hayo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Kauli hiyo ameitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Usagara waliomuomba kusikiliza kero zao ambazo alikubali na kuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wa Idara zote kuhudhulia mkutano huo ili kutoa ufafanuzi na majibu ya kero na hoja mbalimbali za wananchi.
Kitwanga kwanza aliwataka wananchi hao kuwa huru kumuelezea kero zao ili kuwezesha watalamu wa Halmashauri akiwemo nay eye kuanza kuzitolea ufafanuzi na majibu ambapo Mariam Makwaya mkazi wa kijiji cha Sanjo alihoji lini vijiji vya Sanjo na Usagara vitapatiwa maji safi na salama. 

Huku Samwel Malongo akiwatuhumu maafisa ardhi kuvamia kwa kufika katika mashamba yao na kuanza kupima viwanja bila kuwashirikisha na kuwapa taarifa ambapo wamekuwa wakija na watu ambao huwatambulisha kuwa Wawekezaji jambo ambalo limeonekana kulalamikiwa na wananchi wengi .
Kitwanga  alimwomba Kaimu Afisa Ardhi aliyekuwepo katika mkutano huo, Julius Karumuna, kujibu hoja hiyo na alipoanza kujibu wananchi walidai wamefanya hivyo bila kuwashirikisha na hatua ambayo wenyeviti wa vijiji vitano nao waliunga mkono na kudai kuwa husikia tu tayari wakiendelea na upimaji.
Kitwanga alisimama na kumwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Lucas Kulliani na Kaimu Afisa Ardhi, Karumuna kuacha mara moja kuvamia na kupima mashamba ya wananchi kwa kisingizio cha wawekezaji bila kuwashirikisha wananchi ikiwemo kuwalipa fidia inayostahiki kabla ya kuwagawia wawekezaji.
“Kuanzia leo hii ni marufuku kwenda kwenye maeneo na mashamba ya wananchi na kuanza kupima viwanja kwa kisingizio cha kuwagawia Wawekezaji lakini hebu wapeni taarifa viongozi wa vitongoji, vijiji na Kata pia muwashirikishe wenye maeneo yao kabla ya kufanya upimaji mkikubaliana basi mwendelee na uwepo ushahidi,”alisema.
Kitwanga aliahidi wananchi hao kuwa mradi mkubwa na wa uhakika wa maji safi na salama utatekelezwa kama ilivyoahidiwa na Rais Dk  John Magufuli, wakati wa kampeni  katika Mji wa Misungwi ambapo utafika hadi Kata ya Usagara, lakini pia amewataka wananchi kuendelea kumpatia ushirikiano ili kutekeleza ahadi zake na Ilani ya CCM kwa wao pia kuhudhulia mikutano ya Mbunge na Madiwani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.