ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 16, 2016

MWILI WA MWANAFUNZI ALIYE SOMBWA NA MAFURIKO MWANZA WAPATIKANA.

Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wakitoka eneo la  Kamanga Feri jijini hapa, huku wakiwa wameubeba mwili wa mtoto Janeth James (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mabatini uliopatikana mara baada ya wavuvi kuuona ukielea kando kando ya ziwa Victoria eneo la Kamanga Feri. 
Juzi Marehemu Janeth alisombwa na maji wakati akivuka eneo dogo la mfereji unaotiririsha maji na kuingia mto mirongo na maji yake kuelekea Ziwa Victoria, wakati akiwa ameongozana na baba yake mzazi kutoka shule ambako ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria mara baada ya kujiandikisha.

Wavuvi hao wanaeleza kuwa waliuona mwili wa mtoto huyo ukielea, na kutokana na taarifa za kuzama kwake walizozipata kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo Jembe Fm, pamoja na taarifa za wasimamizi wao kibiashara kwenye mwalo huo nao hawakusita kutoa taarifa haraka kwa jeshi la polisi kwaajili ya hatua zaidi.
Licha ya jitihada kubwa za wananchi na majirani wenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatikana mapema tangu siku alipo sombwa na maji na kuzama kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba hatimaye leo ikiwa ni siku ya tatu mwili wa mtoto huyo unaibuka kando kando ya Ziwa Victoria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.