ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 14, 2016

WAZEE,VIONGOZI WA DINI,WAGANGA WA JADI NA WALEMAVU WAKUTANA NA MZINDAKAYA.

Na Shushu Joel,Busega.
MKUU wa wilaya ya Busega , Mkoana Simiyu Paul Mzindakaya amewataka wananchi wake wa Busega kuweza kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini katika suala zima la kupiga hatua katika maendeleo ili  waweze   kujiongezea   kipato katika maisha yao na familia zao.

Hayo yamezungumzwa kwenye kikao chake cha mwanzo wa mwaka na wazee na waganga wa jadi viongozi wa dini  na walemavu wilayani humo, kikao hicho kilikuwa na malengo ya kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo changamoto zao zinazowakabili watu hao katika utendaji wa shughuli zao ndani na nje ya wilaya hiyo.

Mkuu huyo wa wilaiya hiyo aliqwataka wazee,waganga wa jadi na walemavu wa aina zote kutoteteleka katika kazi zao kwani sasa ni hivi ni kipindi cha hapa kazi tu ambayo ni kauli mbiu ya Rais wetu inazidi kuwa na kasi ya pekee kwa watanzania, hivyo wale wasiojishughulisha na kazi watakuwa awawezi kuendana na kasi ya wilaya yetu.

Aliongeza kuwa anawataka wazee na viongozi wa dini na wengine ambao ni wakuu wa familiakuweza kuwa wasemaji wakuu kwa vijana wetu ambao wanaonekana kuwa ni gumzo katika jamii yetu hasa katika shughuli za maendeleo yao kwani vijana wengi wamekuwa ni wachezaji wa kamali na wacheza mapuru table kwa muda mwingi hivyo hata kujihusisha na masuala ya maendeleo yao wanashindwa nah ii ni kutokana na tama za kupata mali mapema.

Aidha amewataka vijana wote wa Busega kuweza kuunda vikundi ili Halmashauri iweze kuwapatia mikopo kwa ajili ya shughuli za maendeleo yao ili waweze kujikwamua katika maisha yao hivyo waje ofisini muda wowote ule lakini wawe na masuala ya maendeleo ili wasikae kuwa wanailaumu serikali juu ya ajirana huku wao awataki kujishighulisha na kazi za kawaida.

Kwa upande wake Mzee Petro Mabeyo(87) mkazi wa kata ya kiloleli amempongeza mkuu wa wilaya kwa kutambua umuhimu wa wazee ndani ya wilaya yake, pia tunakushukuru kwa agizo lako la kumtaka mganga mkuu anaanza mara moja kuhakikisha wazee wasiokuwa na vitambulisho vya matibabu bure wanapewa haraka sana ili nao waeze kupata huduma za bure kama wengine.

Na kwa upande wa mwakilishi wa waganga wa jadi Saimon Ndila alisema kuwa kilio chao kwa serikali ni kutokupewa lessen za kuweza kuendeshea kazi zao hivyo wamemtaka mkuu wa wilaya kuweza kuwasaidia ili waweze kupata lessen hizo alisema.

Aliongeza kuwa wanaiomba serikali kuweza kuwa na imani na waganga wa jadi kwani si wote wanaofanya kazi hiyo ni wale wanaowadanganya watu juu ya utajiri mara wapelekapo viungo vya walemavu wa ngozi na kuitaka serikali kuwa punde wanapowabaini waganga wa namna hiyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.