Wananchi wamedai kuwa mvua hiyo, iliyonyesha kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri, haijawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne iliyopita.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabatini, Ntobi Ntobi pamoja na kaimu kamanda wa kikosi cha Zimamoto jijini Mwanza, Hamidu Nguya walithibitisha kutokea kwa kifo cha mtoto huyo, Jenipher Joseph (6), aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini.
Kamanda Nguya alisema mtoto huyo alisombwa na maji na baba yake, James Joseph walipoteleza na kuangukia mtoni wakati wakivuka daraja la Mto Mirongo uliokuwa umefurika.
Mvua Yauwa Mtoto 1 Mwanza
Fuatilia taarifa hii iliyoandaliwa na Star TV. Mwanza.Mkazi wa Mabatini jijini Mwanza akijiokoa kwa kupanda juu ya bati, baada ya eneo lao kukumbwa na mafuriko ya maji kutokana na mvua iliyonyesha jana jijini humo. Picha na Michael Jamson. |
Miongoni mwa waliopoteza mali ni pamoja na Juma Said, mmiliki wa duka la vifaa vya shule na ofisi zenye thamani ya zaidi ya Sh7.5 milioni.
Hadi saa wakati tunatoka eneo la tukio, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa kikiendelea na juhudi za uokoaji na kutafuta miili ya watu wanaodhaniwa kuwa wamesombwa na mafuriko hayo.
Huu mchanga na tope umejikita hapa na kusababisha barabara kupitia kwa shida. |
Hali tete juhudi zimekwama..... |
Mitaani nako si salama. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.