Kwa siku ya leo imekuwa ni kama mwendelezo watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo wameonekana wakihangaika huku na kule kuhamisha vifaa vyao kutoka katika nyumba hizo.
Wengine wakifanya mikakati ya hamahama.
Kutokana na bomoa bomoa inayoendelea Eneo la Ghana kwa sasa limekatiwa umeme hali inayosababisha ulinzi wa mali kuwa mgumu, usiku mzima wananchi hao wamekesha kulinda mali zao kwani vibaka walikuwa wakilandalanda kuiba mali zilizonje ya magofu ya nyumba zilizobomolewa sambamba na kung’oa flemu za milango na madirisha.
Wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia maturubai kwa ajili ya kujisitiri wakati wakiwa katika harakati ya kutafuta sehemu nyingine ya kupanga.
Hii ndiyo hali.
Huduma za maji tayari zimekwisha sitishwa.
Hapa alikuwa akiishi balozi.
Vibaka nao wamekuwa wakipitia mabati na mengineyo..
Kwaheri mjengo...
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Wilson Kabwe amesema kuwa tayari notisi ya kuhama wakazi hao aliowaita kuwa ni wavamizi ilikwishatolewa kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kwamba kilichokuwa kinasubiriwa ni wao kuhama bila ya kubughudhiwa lakini wakakaidi agizo mpaka bomoabomoa ilipowakuta.
Kabwe, ameongeza kuwa tayari usanifu wa mchoro kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Machinga ulikwishafanyika na soko hilo linajengwa katika eneo hilo la Mtaa wa Ghana, Wilaya ya Ilemela.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.