Baadhi ya matokeo ambayo mpaka sasa yamekwisha toka kwenye Kata za Igunga ni Kituo cha Bigadilele ambako CCM ilipata kura 135 na Chadema (96), Choma Bwangamila CCM (193) na Chadema (58).
Katika katika kata ya Nanga, yanaonyesha CCM kupata kura 845 dhidi ya 915 za Chadema, CUF 45 ,DP sita, AFP moja, Sau mbili, UPDP tatu na Chausta mbili.
Kwa upande wa matokeo yaliyojumlishwa kwa Kata ya Nkinga yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 1,266, Chadema 1,205, CUF 64 Chausta mbili na AFP mbili.
Matokeo ya Kata ya Bukoko yanaonyesha CCM imepata kura 828, Chadema 726, CUF kura saba, wakati vyama vya SAU, DP, CHAUSTA, AFP na UPDP vikiwa havikupata kitu.
Katika Kata ya Sungwizi, CCM kilikuwa na kura 1,318 huku Chadema kikiwa na kura 671 na CUF kikiambulia kura 14.
Katika Kata ya Simbo, Chadema kinaonekana kuwa mbele kwa kupata kura 861 huku CCM kikiwa na kura 553, CUF 268 na SAU kura moja.
Kwa ujumla, hali ya upigaji kura imekuwa shwari licha ya kuwapo kwa baadhi ya watu waliodai kuyakosa majina yao kwenye vituo.
Mgombea UPDP hakupiga kura
Mgombea ubunge kupitia UPDP, Hemedi Ramadhani Dedu hakupiga kura kwa kuwa hakujiandikisha katika Jimbo la Igunga.
“Sikupiga kura ndugu yangu kwa sababu sikujiandikisha hapa, nimejiandikisha Dar es Salaam.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.