ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 8, 2011

KUELEKEA NYERERE'S DAY BW. JUMA MAKONGORO AKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI IKIZU A.

Mgeni rasmi mwakilishi wa Familia ya Hayati Baba wa Taifa, Bw. Madaraka Nyerere akikata utepe kuzindua mradi wa kuchangia madawati na elimu Shule za mitaa na vijiji vya kata ya Nyamswa na Ikizu ambapo jumla ya madawati 50 yalitolewa jana.

Ndugu Juma Makongoro akikabidhi Madawati 30 kwa Bw. Madaraka Nyerere ambaye aliyawasilisha kwa uongozi wa shule.

Wanafunzi wa Shule ya Ikizu A wakikabidhiwa madawati 20 toka mwakilishi wa Mradi wa Zinduka mkoani Mara.

"Mimi binafsi nilisoma katika shule hii kongwe, lakini kama mtamkumbuka Mwalimu aliyenifundisha darasa la kwanza, marehemu Karemela Diaz kwenye mazishi yake nilipata nafasi ya kutoa ushuhuda wa namna ninavyomfahamu na nikaahidi na kutoa wito kwa Waikizu wote kutafuta njia bora ya kumuenzi. Sasa njia moja wapo tumeianzisha leo..."Says Juma Makongoro.

Naye Mgeni rasmi mwakilishi wa Familia ya Baba wa Taifa Bw. Madaraka Nyerere amesema kuwa kuna haja ya vijana wote waliopita katika shule hiyo kuungana kwa pamoja na kuona ni jinsi gani wanaweza kuifanikisha na kuiwezesha shule hiyo katika hatua zake za maendeleo ya elimu .

Kifimbo ni zawadi kwa madaraka Nyerere toka kwa uongozi wa shule ya Ikizu A.

Mama wa Juma Makongoro akitoa yake.

Wanafunzi wa shule ya Ikizu A na madawati yao 50 waliyokabidhiwa.

Wakiimba wimbo wa shukurani hawa ni wanafunzi wa shule ya ikizu A wilayani Bunda mkoani Mara.

Ngoma ya jadi ya kabila la Waikizu.

Picha ya Pamoja part one.

Makongoro amesema kuwa lengo la msaada huo ni kutaka utumike kama wito kwa jamii yote ya Waikizu kujenga tabia ya kujiletea maendeleo wenyewe badala ya kutegemea nguvu za serikali kwani serikali nayo bado ina mzigo wa majukumu na changamoto nyingi zinazoikabili.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. This is the perfect blog for anybody who wishes
    to find out about this topic. You realize so much its almost hard to argue with you (not that
    I personally would want to…HaHa). You definitely put
    a fresh spin on a topic that's been written about for many years. Wonderful stuff, just great!

    Have a look at my blog :: magic flight launch box

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.