TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, leo imewafikisha mahakamani waliokuwa viongozi waandamizi wa Chama Kikuu cha Shirika, Nyanza Cooperative Union (NCU), kwa tuhuma za ubadhirifu na ufujaji wa mali.
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Susan Mwendi amesema, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU umeeleza kuwa aliyekuwa Mwenyekiti Jacob Shibiliti na Makamu wake John Magulu ilibainika kati ya Januari 1, 2003 hadi Desemba 31, 2004 waliisababishia hasara NCU jumla ya Tshs.426,400,000 kwa kipindi hicho huku Makamu Mwenyekiti aliisababishia hasara shirika hilo takribani Tshs.332,640,000.
Mwendi amesema kuwa watuhumiwa waliisababishia NCU, hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza pamoja na kifungu cha 57(1) na 60(2) vya sheria ya Uhujumi uchumi, sura ya 200 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.