Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye alisimama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akimpokelea fomu Mkuu wa Mkoa ushiriki wa mbio za Rock City Marathon. |
Na Albert G. Sengo Mwanza.
MARA baada ya Kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon 2013 hii leo kutangaza usajili rasmi kwa washiriki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ametangaza kushiriki mbio hizo kutokana na umaarufu wake maeneo mengi Kanda ya Ziwa.
Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba ,2013 katika uwanja wa CCM Kirumba na tayari watu wengi wameanza kuchukua fomu ili kushiriki.
Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye alisimama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akipokea jezi atakayo vaa Mkuu wa Mkoa siku ya ushindani mbio za Rock City Marathon. |
Ndikilo ambaye aliwakilishwa na, Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko, mbali na kuipongeza kampuni ya Capital Plus International ambayo ni mwaandaji wa mbio hizo, alitoa wito kwa viongozi wa chama cha Riadha Mkoani Mwanza, waratibu na wasimamizi wa michezo wilayani na Mkoa wa Mwanza kuongeza nguvu katika kuhamasisha ushiriki wa watu ili mkoa huo uweze kuvumbua na kuinua vipaji vipya katika riadha.
“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), African Barrick Gold, Precision Air, Airtel, Bank M, Parastal Pensions Fund (PPF), Nyanza Bottlers, New Mwanza Hotel, Sahara Communication na Umoja Swithch ambao wamejitokeza kuunga mkono jitihada hizi ambazo zitasaidia kuinua mchezo wa riadha nchini pamoja na kutangaza nchi yetu,” alisema.
Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo kuelekea Rock City Marathon. |
“Tumeshuhudia wanariadha mbali mbali vijana wa nchi kama Kenya wakiibuka washindi katika mbio zilizofanyika mjini Berlin, Ujerumani hivi karibuni na kujinyakulia fedha nyingi pamoja na zawadi mbali mbali. Hii iwe chachu kwetu kama mkoa na Taifa kwa ujumla kutilia mkazo mchezo huu kwani licha ya kuwa ni ajira kwa vijana lakini pia zinatumika kama kitambulisho kikubwa cha taifa letu kimataifa endapo wanariadha wetu wataweza kufanya vizuri,” alisema Ndikilo.
Picha ya pamoja ya wadauna wadhamini wa Rock City Marathon 2013. |
Mratibu wa mbio hizo Mathew Kasonta . |
“Kwa wale watakao tumia Airtel Money
kujisajili, unapaswa kutuma pesa kwa jina la fumbo (MARATHON) ambapo utapokea
ujumbe utakaouonyesha pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi
za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha
na Mwanza,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza Silas Nkungu akizungumza na waandishi wa habari. |
Alibainisha kuwa fomu za usajili
zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km
21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na
taasisi).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.