DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.
Na Mwandishi Wetu,
Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo
la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa
na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia
ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK. C.S Muthukumaran,
mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.
(VSD) ni tundu katika ukuta
unaotenganisha ventriko ya upande wa kulia na kushoto katika moyo. Ni tatizo
linalotokea mara nyingi wakati wa kuzaliwa kwa mtoto na linaweza tokea lenyewe
au kama ugonjwa.
Ni kawaida kwa watoto wote kuzaliwa
na tundu dogo katikati ya atria mbili na mara nyingi tundu hilo huziba ndani ya
wiki chache. Mara nyingi hakuna tundu kati ya ventiko hizo mbili, ila baadhi ya
vichanga huzaliwa na tundu hilo ambalo linakuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo
na ndio sababu kubwa ya watoto wachanga
wengi kuonana na wataalamu wa magonjwa ya moyo.
Imezoeleka mara zote kuziba tundu
hili kwa upasuaji wa moyo (operesheni), ambao unahusisha kupasua kifua, kupitisha
mashine na kuziba tundu hilo. Kwa mujibu wa DK. Muthukumaran kwa
miaka 10 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa ya kutibu tatizo hili ambapo hospitali za Apollo wamegundua njia ya
kuziba tundu hilo kwa kutumia njia ya “pini kwenye tundu” (angiogram) bila kovu
lolote kifuani. Licha baadhi ya aina za tundu hilo kwenye moyo kama lile
lililopo chini ya valvu za moyo ni lazima lizibwe kwa upasuaji. Makala hii
inaonyesha jinsi gani tundu hilo katika moyo linaweza kuzibwa bila upasuaji au
wowote.
Mtoto wa kike wa umri wa miaka 12
amekuwa na tatizo la moyo. Aligundulika akiwa na tundu katika moyo akiwa na
umri wa miaka miwili. Madaktari walishauri afanyiwe upasuaji kwa sababu tundu lilikuwa
karibu sana na valvu hivyo ingeweza kuharibu valvu ya moyo. Wazazi wake
waliogopa suala la binti yao kufanyiwa upasuaji huo ambao ungeweza kusababisha
apoteze maisha lakini pia kuwa na kovu kubwa kifuani. Waliahirisha upasuaji huo
mpaka pale binti alipofikisha umri wa miaka 14. Kwa umri huo tayari lile tundu
lilikuwa limeshaanza kuharibu ile valvu iliyokuwa karibu nalo.
Wazazi walikwenda hospitali ya watoto Apollo kwa ajili ya
ushauri mwezi Septemba 2014. Baada ya
utafiti wa kwanza madkatari walisema wanashauri tundu lile lizibwe kwa njia ya
“pini” bila kufanya upasuaji. Baada ya wazazi kuelewa, walimchukua mtoto kwa
ajili ya maandalizi. Hatua za maandalizi zilifanywa mtoto akiwa katika nusu
kaputi (local anaesthesia). Hatua hizo zilichukua nusu saa tu. Tundu hilo
lilizibwa kwa mafanikio makubwa kwa njia ya pini na katheta na mgonjwa
aliruhusiwa kutoka hospitalini siku iliyofuata. Familia ilifurahi sana, kwa
jinsi walivyotua mzigo mkubwa wa tatizo hilo la binti yao wa miaka 14.
Wakati wa ufuatiliaji wa maendeleo
kwa muda wa mwaka mmoja, binti alikuwa akiendelea vizuri, hakukuwa na uvujaji
wowote wala tatizo katika aortic na valvu za upumuaji. Tiba hii ya siku moja
imemwezesha binti huyu kuepuka upasuaji katika mfumo wake wa upumuaji, kovu
kubwa la maisha yake kifuani na siku 5-6 za kulala hospitali kwa ajili ya
upasuaji.
Uzibaji wa tundu katika moyo umekuwa
ukifanywa kwa mafanikio kwa muda wa miongo miwili. Ufuatiliaji wa
maendeleo kwa muda mrefu umeonyesha kuwa
uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia hii mpya ijulikanayo kitaalamu kama
‘Transcatheter’ ni mbadala bora wa kuepuka upasuaji. Kwa kipindi kirefu
upasuaji umekua njia pekee ya kuziba tundu katika moyo. Ila ina kuwa hatarishi
mara kadhaa hasa moyo kuziba kabisa, baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara
moja na hata vifo. Zaidi ya yote, matatizo ya maambukizi, mfumo wa fahamu na
mapigo ya moyo kwenda kasi zaidi (tachyarrhythmia). Baada ya kufanyiwa
upasuaji, kovu litadumu maisha yote. Hivyo kwa njia ya hii mpya ya kuziba tundu
ni bora na salama kwa afya ya baadae.
Dk.
C.S Muthukumaran ametoa maoni yake kwamba, kurithi ni moja kati ya
sababu kubwa za kusababisha tundu katika moyo. Kwa mfano, mzazi mwenye tatizo
la tundu kwenye moyo ana nafasi kubwa ya kupata mtoto mwenye hali hiyo zaidi ya
mazazi asiye na tatizo hilo. Watoto wenye maradhi ya kurithi kama utindio wa
ubongo mara nyingi huwa na tundu katika moyo. Uvutaji sigara kipindi cha
ujauzito kwa mama kumehusishwa pia kama chanzo cha matatizo haya ya tundu
katika moyo wa mtoto.
Kama tatizo hilo la tundu katika moyo
lisipopatiwa matibabu huwa linaweza kusababisha matatizo ya moyo, anasema Dk. Muthukumaran. Ukuaji wa tundu hilo
katika moyo inaweza kusababisha moyo kushindwa kuendelea kusukuma damu, au kuwa
na mapigo yasiyo sahihi, kudumaa kwa mwili hasa kwa watoto wachanga. Mtoto
anashindwa kula sawa sawa na hivyo kuathiri ukuaji wake. Na matokeao yake mtoto
anapungua uzito au asikue kabisa.
Katika hospitali ya watoto ya Apollo uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia
ya Transcatheter umefanywa kwa zaidi ya
watoto 300 kwa miaka 5 iliyopita kwa kutokuwa na matatizo yoyote makubwa. Zaidi
ya 50% ya matatizo ya tundu la saizi ndogo mpaka yale ya wastani yamezibwa kwa
njia hiyo kuingiza katheta. Ujuzi mkubwa wa madaktari, uchaguzi sahihi wa
wagonjwa, mipango sawia ndio ufunguo wa mafanikio katika njia hii ya kisasa.
Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali za Apollo ni za kwanza
katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa
Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji
kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma
bora kwa wagonjwa. Taasisi ina wataalamu waliobobea
kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu
vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na
vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika
teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology),
magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na
matatizo ya uti wa mgongo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.