Katika mchezo wa leo, Simba SC ilipata pigo mapema tu dakika ya 24, baada ya beki wake wa kati, Abdi Banda kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na refa Jonesia Rukyaa wa Kagera kwa kumchezea rafu Ngoma.
Mshambuliaji wa Zimbabwe, Ngoma akaifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya 39, akitumia makosa ya beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Kessy aliyemrudishia pasi fupi kipa wake Vincent Angban raia wa Ivory Coast.
Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, baada ya kusajiliwa kutoka Platinum FC ya kwao, aliiwahi pasi ya Kessy kabla haijamfikia Angban na kumlamba chenga kipa kisha kufunga.
Simba SC walitulia baada ya bao hilo na kucheza kwa tahadhari, wakiendelea kushambulia langoni mwa Yanga SC na kupata kona mfululizo, ambazo hawakuweza kuzitumia kupata bao.
Kipindi cha pili, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mganda, Jackson Mayanja kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza beki Nova Lufunga, yaliidhoofisha safu ya kiungo ya timu hiyo na kuwafanya Yanga waanze kutawala mchezo.
Krosi maridadi ya winga Godfrey Mwashiuya kutoka upande wa kushoto iliunganishwa nyavuni kwa guu la kulia na Mrundi Tambwe dakika ya 72 kuipatia Yanga SC bao la pili.
Pamoja na kuwa nyuma kwa 2-0, Simba SC waliendelea kufikisha mipira kwenye eneo la hatari la Yanga, lakini hata hivyo leo safu yake ya ulinzi iliyoongozwa na Vincent Bossou na Mbuyu Twite ilikuwa makini.
Vikosi vilikuwa;
Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk64, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima/Simon Msuva dk52.
Simba SC: Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Abdi Banda, Justice Majabvi, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Novat Lufunga dk46, Hamisi Kiiza/Danny Lyanga dk59,Ibrahim Hajib/Brian Majwega dk80 na Said Ndemla.
MWANZA
Kipute cha dimba la CCM Kirumba Mwanza ni Toto Vs Kagera Sugar 1-1. |
Kocha wa timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza John Tegete akizungumza na waaandishi wa habari baada ya mchezo. |
Azam FC imeichapa Mbeya City maabo 3-0 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabao ya Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco na Farid Mussa.
Azam FC inafikisha pointi 45 kwa ushindi huo, baada ya kucheza mechi 18 na kupanda hadi nafasi ya pili, ikiizidi Simba kwa wastani wa mabao.
Mechi nyingine; Mgambo JKT imetoa sare ya 1-1 na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Stand United imetoka 1-1 na JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.